Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Hakuna aliyetarajia kuwa Mbowe angekosa hekima katika kufikia maamuzi ya ama kugombea au kupumzika, mpaka iliposhuhudiwa leo.
1. Kwa kuzingatia misingi ya demokrasia, Lisu alistahili kushindani katika nafasi anayogombea, lakini mpinzani huyo hakustahili kuwa MBOWE.
2. Mbowe, kiuhalisia, hata kuwepo kwenye nafasi hiyo kwa miaka 21, tayari ame-over stay. Angekuwa na hekima asingeendelea kuing'ang'ania nafasi hiyo tena.
3. Wanachama na wapenzi wengi wa CHADEMA, wataanza kumwona Mbowe kuwa ni adui mkubwa wa demokrasia, mbinafsi anayeamini kuwa hakuna mtu mwenye uwezo kama wa kwake au kumzidi yeye.
4. Kung'ang'ania kwake madaraka kunapeleka ujumbe muhimu kwa wananchi kwamba Mbowe alipokuwa anasema kuwa uongozi kwenye vyama vya upinzani ni mateso, labda anaongelea watu wengine, lakini kwake binafsi, uongozi huo unamnufaisha na kumfaidisha. Kiuhalisia ni kwamba huwezi kung'ang'ania mateso. Tena akitokea mwingine kuwa tayari kuyabeba hayo mateso, utashukuru sana.
5. Mvurugano na mpasuko alioutengeneza Mbowe ndani ya CHADEMA, unaimaliza CHADEMA, hivyo wanachama wa CHADEMA ambao waliitaka CHADEMA iwe na nguvu zaidi ili kupambana na CCM, watamchukia Mbowe kwa kiwango ambacho hakukitarajia. Mbowe atageuka kuwa adui mkubwa wa wanachama wa CHADEMA, naye atakuwa rafiki mkubwa wa CCM, japo kwa siri, kwa maana ameweza kusaidia kufanikisha malengo ya CCM ya kuua upinzani. Lakini asichokijua ni kuwa baada ya kuisaidia CCM kuiua CHADEMA, CCM hawatakuwa na muda naye kwa sababu CHADEMA haitakuwa threat wala kuwa competitor. CCM itaelekeza nguvu zake kwa kiongozi atakayekuwa akiongoza chama cha upinzani chenye nguvu, inaweza kuwa ni CHAUMA au ACT, kama Lisu atahamia kwenye chama kimojawapo. Itakapofikia hatua hiyo, Mbowe atapozwa na cheo cha Parole, kama ilivyokuwa kwa marehemu Mrema.