Watakaoiba vibao vya makazi kuwa chuma chakavu wapewa onyo kali

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Sunday Deogratias ametoa onyo kwa watu watakao onekana kung'oa vibao vya anuani ya makazi na kwenda kuuza kama vyuma chakavu na kwa watakaobainikia watachukuliwa hatua za kisheria.

Hayo ameyasema alipokuwa katika hafla ya siku ya wanawake wilayani humo na kuongeza kuwa kuna mikoa ambayo zoezi hili la vibao vya makazi tayari lilifanyika lakini watu waling'oa vibao na kuviuza hivyo katika Halmashauri yake hatarajii jambo hilo litokee ambapo amewataka viongozi wote wa ngazi ya kata na vijiji pamoja na wananchi kuvilinda vibao hivyo ili visiharibiwe.

"Viongozi wote wa kata na vijiji ninaomba mkahakikishe vibao hivi vinakaa katika hali ya usalama, nanyi wananchi mnatakiwa kila mmoja awe mlinzi wa mwenzie ili kuhakikisha Halmashauri yetu inakaa katika mpangilio mzuri wa mitaa," Amesema Mkurugenzi.

“Tunataka tutambue nyumba na barabara zetu, mfano unaweza kuagiza kitu mtandaoni unaletewa hadi nyumbani kwako.”

Source: Wasafi FM
 
Picha ipo wapi? Tusubir ripoti ya CAG utashuhudia upigaji
 
Vibao kuwa Chuma chakavu?
 
Safi maana chuma stend za daladala wameiba hadi aibu
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Sunday Deogratias ametoa onyo kwa watu watakao onekana kung'oa vibao vya anuani ya makazi na kwenda kuuza kama vyuma chakavu na kwa watakaobainikia watachukuliwa hatua za kisheria.

Hayo ameyasema alipokuwa katika hafla ya siku ya wanawake wilayani humo na kuongeza kuwa kuna mikoa ambayo zoezi hili la vibao vya makazi tayari lilifanyika lakini watu waling'oa vibao na kuviuza hivyo katika Halmashauri yake hatarajii jambo hilo litokee ambapo amewataka viongozi wote wa ngazi ya kata na vijiji pamoja na wananchi kuvilinda vibao hivyo ili visiharibiwe.

"Viongozi wote wa kata na vijiji ninaomba mkahakikishe vibao hivi vinakaa katika hali ya usalama, nanyi wananchi mnatakiwa kila mmoja awe mlinzi wa mwenzie ili kuhakikisha Halmashauri yetu inakaa katika mpangilio mzuri wa mitaa," Amesema Mkurugenzi.

“Tunataka tutambue nyumba na barabara zetu, mfano unaweza kuagiza kitu mtandaoni unaletewa hadi nyumbani kwako.”

Source: Wasafi FM
Unataka Wakale wapi na Ajira hakuna?
 
Ajira ajira ajira ajira ajira

Kitu kilichoshindwa kuuzika ni Chuma cha reli tu,, vingine hvo waandae magereza
 
Si watumie plastik ngumu tu mbona inawezekana.
 
Ndo madhara ya kufakamia double kik hayo, Hadi vibao vya anuani za makazi yao wanaiba.
 
Back
Top Bottom