Watakaopata daraja la 4 na sifuri elimu ya sekondari watashtakiwa kwa uhujumu uchumi

Watakaopata daraja la 4 na sifuri elimu ya sekondari watashtakiwa kwa uhujumu uchumi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Afisa Elimu wa Mkoa Kilimanjaro, Paulina Mkwama amesema watakaopata chini ya Division 3 wajiandae kushtakiwa kwa uhujumi Uchumi.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Umbwe walipokuwa katika ziara ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Gerald Mweri.

Amesisitiza kuwa Serikali inagharamia kwa kulipa mishahara walimu na watumishi wa elimu halafu wakapata division 4 au sifuri, haikubaliki na wajiandae kushtakiwa kwa uhujumu uchumi.

Shule ya Sekondari ilikuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 kutokana na uchakavu wa mabweni ambapo sasa imekarabatiwa hivyo itaweza kuchukua wanafunzi 700.

 
Kha jamani, si bora kutoa motisha kwa watakao faulu wapewe zawadi, sasa hivi vitisho vya nini.

Wataalam wa sheria tunaomba ufafanuzi
 
Hivi kufeli mtihani ni kosa la jinai ?
Au ni la madai ?
Au ni kosa la kinidhamu ?

Mbona mimi naona kama sio kosa.
 
Ikiwezekana walipe na faini 100M sana iwe fundisho kwa wazazi wajue faida ya upinzani bungeni.
 
Akija mgeni toka Burundi Leo halafu afungulie tiivii akute habari ya kwanza Ni hii ya Mkwama.
Habari ya pili Ni waziri wa elimu akiwafokea wachina kwa kiingereza, habari ya tatu Ni waziri wa nishati akisema ambao watakua hawajafungiwa umeme watapelekwa polisi, habari ya nne Ni mh. Chala Mila akiongea kuhusu kumbusu mtu ambae humjui, habari ya tano Ni bungeni ambapo mbunge mmoja anaongelea kuhusu large sex payers na Ile ya building and Finance na ya mwisho Ni mzee Halima akiapishwa.
 
Huyu aliyetoa hii kauli alipata daraja gani (nina uhakika kwa upeo na fikra hizi) hata kama alipata four na sio sifuri aliiba mtihani / aliangalizia au mitihani yetu haipimi fikra za mtu bali kukariri

Ningeomba anyanganywe vyeti vyote alivyopata sababu ameweka shule yake aliyosoma katika disrepute
 
Uhujumu uchumi, moja ya makosa ambayo kupata dhamana ni mtiti! Sijaelewa, anataka wazazi wahamishie watoto wao shule za private huyu nini? Au ana hisa kwenye shule za Binafsi!? Motisha za vitisho hazifanyi kazi sawasawa sehemu zote!
 
Afisa Elimu Mkoa wa Kilimanjaro, Paulina Mkwama amesema wanafunzi watakaopata daraja la nne na sifuri (Division 4 & 0) katika shule ya sekondari ya Wavulana ya Umbwe wajiandaw kushitakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi. Amesema kwamba haiwezekani mwanafunzi usomeshwe na serikali kwa kutumia hela za serikali halafu utegemee kupata Division 4 au 0.
 
Afisa Elimu wa Mkoa Kilimanjaro, Paulina Mkwama amesema watakaopata chini ya Division 3 wajiandae kushtakiwa kwa uhujumi Uchumi.
Huyu akamatwe na kuchukuliwa hatua kwakuwa amezua taharuki kwa watoto badala ya kuelekeza akili kusoma yeye amewajengea hofu na hivyo hawatasoma kwa amani
 
Back
Top Bottom