Watalaamu Wa Sheria Msaada

Watalaamu Wa Sheria Msaada

Tumbo Tumbo

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
1,278
Reaction score
1,553
Naomba kuuliza kisheria/ Legally; ukiwa unafanya kazi kwa niaba ya Taasisi iliyokuajiri na kisha ukakosea katika utendaji wako (kwa capacity ya Taasisi not personal); swali langu ni je, unastahili kuadhibiwa kibinafsi au inastahili kuadhibiwa Taasisi kisha wewe binafsi ukawajibika kwa mujibu wa taratibu za Taasisi kv kwa kosa la kuitia taasisi hasara au kuiondolea Taasisi reputation nzuri mbele ya Umma...??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali lako lina'base' zaidi katika sheria ya mikataba sura ya 345 ya sheria za tanzania na jambo lako linaangukia moja kwa moja katika sehemu ya X ya sheria hiyo.
Katika masuala ya AGENCY,agent huwa anafanya kazi kwa niaba ya principle na hicho kitu kilichofanywa huhesabiwa kuwa kimefanywa na principle mwenyewe.
Kuna masharti/vigezo ambavyo huatkiwa kuzingatiwa hasa na agent pale anapokuwa anafanya kazi ya uwakilishi ambayoyametolewa na sheria hii nayo ni kwamba agent anatakiwa kufanya shughuli halali pale anapopata hayo madaraka yake {kifungu cha 140(1),(2)}. Hii ina maana kwamba agent akifanya shughuli zilizo kinyume na sheria hasa na mipaka yake kulingana na mkataba wake na principle, basi hilo litakua ni kosa lake binafsi. Pia kigezo kingine kinachotakiwa kuzingatiwa na agent ni kwamba pale inapotokea dharula ya namna yoyote, basi anayo mamlaka kamili katika kuzuia/kuepusha ajali au hasara yoyote ambayo ingeweza ktokea kutokana na dharula hiyo lakini kiwango cha uepushaji wa hasara hiyo kiwe ni sawa na kile ambacho mtu mwenye akili/uelewa sawa anaweza kufanya.{kifungu cha 140 na 141}
Jambo kubwa na la muhimu la kuzingaiwa hapa nikwamba agent anatakiwa kuzingatia mkataba wake na priciple yyani azingatie mipaka yake, na kama kuna tatizo ambalo litatokea kutokana na agent kuzingatia mkataba na halitokani na kifungu cha 141 cha sheria hii, basi PRINCIPLE NDIYE ATAWAJIBIKA kwa tatizo hilo.

BAADA YA UTANGULIZI HUO, TURUDI KATIKA SWALI LAKO LA MSINGI.
Jibu ni hapana, agent hawezi kuwajibika kwa kigezo cha yeye kuzingatia mkataba na hasara(damage) ikatokea kutokana na agent kuzingatia mkataba (yyani maelekezo aliyopewa na principle). Muwajibikaji katika hili atakua ni principle mwenyewe.
KIPI UFANYE SASA?
1. Kama ikitokea hatua za kimahakama zimechukuliwa dhidi yako na mtu uliyemsababishia hasara (third party) kutokana na uwakilishi wako mwema, basi utaiomba mahakama imuunganishe na principle wako katika shauri hilo la madai. Hili unaweza kulifanya wewe mwenyewe kwa kumtafuta wakili.
2. Kama principle ndiye amekuchukulia hatua kwa kosa la kumsababishia hasara, basi nenda kamfungulie shtaka la madai katika baraza la kazi au mahakamani kutokana na mkataba wenu unavyoonesha.

I STAND TO BE CORRECTED
ASANTE. Nimetoa maoni hayo kutokana na taarifa zilizopatikana kutoka katika swali lako, kwa taarifa ambazo hazijaoneshwa, sitawajibika kwa hizo.
 
Back
Top Bottom