Watambue wachezaji wasio na wanaotambua vipaji na thamani zao

DITOPILE WAPILI

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2015
Posts
384
Reaction score
261
Deo Kanda ni mchezaji aliyetokea TP-Mazembe ya CONGO, kuja kucheza mpira Club ya Simba ya Tanzania.

TP-Mazembe ni moja katika timu tajiri na bora katika bara la Afrika na imekwisha chukua vikombe mara kadhaa vya bara Afrika.

Deo Kanda anaondoka TP Mazembe, akiwa na mshahara mzuri tu, kuja simba kwa mkopo sababu kubwa alikuwa hana nafasi ya kucheza wala kuanza katika kikosi cha kwanza katika Club ya TP-Mazembe, ndiyo maana sasa hivi yupo katika kikosi cha Simba.

Ndani ya Kikosi cha Simba Deo Kanda amekuwa LULU na mtamu kama mcharo, pia kuna tetesi kuwa TP-Mazembe wanamtaka tena Deo Kanda, lakini Deo Kanda hayupo tayari kuondoka Simba anafurahi maisha ya kuwa Simba pamoja ufalme na thamani aliyopewa club ya wekundu hao wamsimbazi.

Ibrahimu Ajibu Mzee wa makorokocho, mguu wa dhahabu majina hayo na sifa aliyapata alipokuwa kapteni wa Timu ya Yanga.

Lakini kutokana na Yanga kuyumba kiuchumi, na ushawishi wa fedha "MO" Ajibu anakwenda kujiunga na Club ya Simba.

Ndani ya Club ya Simba kutokana na wachezaji wanaunda kikosi hicho, Ajibu hana namba ya kucheza hata kwenye kombe la mapinduzi.

Wachezaji wengine waliotoka Club kubwa kuja kucheza ligi yetu ya bongo kwa sababu ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza ni Bernard Morrison raia wa Ghana aliyetokea Afrika ya Kusini timu ya Orlando Pirates.

Sasa hivi Bernard Morrison amekuwa mfalme ndani ya Yanga, huku Gadiel Michael na Beno Kakolanya wanaendelea kukalia mbao katika timu ya Simba.

Kwa akili hizi wachezaji wetu watasugua sana benchi, wanashindwa kutambua kwamba thamani yao inalindwa kwa kucheza mpira, sio kupokea mshahara.

Sipati picha mchezaji wa kutengemewa na club pamoja na timu ya taifa anatoka kwenye timu ambayo anao uhakika wa kuanza kwenye kikosi cha Kwanza na kucheza mechi zaidi ya asilimia 90%, kwenda kwenye timu ambayo hata kwenye wachezaji wa akiba hayumo kabisa.

Haya sasa kwa tamaa ya fedha endelea kusugua bechi, kipaji kinakwisha na muda nao sio rafiki sana.
 
Huwa mnawamiss kina Ajibu eee. Kila siku mnafungua nyuzi mpya kuwazungumzia wao tu.
Kila mtu anaangalia maisha yake. Deo kanda asha win kila kitu akiwa na Mazembe, CAF championship
League ya Kongo Ajibu hajawahi shinda league, Gadiel vilevile, ko wanatafuta mafanikio usiwashangae.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajuaje kama hao uliowataja wangekuwa kwenye mipango ya kocha wenu mpya? Yondani mpo nae na hamkuwahi kuwaza kuwa kuna kocha anaweza kumuweka benchi lakini mbona mnaona kawaida.

Wachezaji walioenda simba ilikuwa first 11 ya zahera na alishaondoka na huwezi kuthibitisha kuwa hao wachezaji wote bado wangeendelea kuwa wachezaji tegemeo hapo yanga chini ya kocha mpya, sasa malalamiko ya nini?
 
Ukijaji hoja yangu kwa kuweka usimba na uyanga, UTAKUWA UMEKOSEA SANA

Mimi nimechukulia tabia ya wachezaji wetu kwa ujumla kutotambua thamani na vipaji vyao.

mfano mwingine MAALIMU BUSUNGU alikuwa bonge la mchezaji alipokuwa Mgambo, tena alikuwa mpaka timu ya taifa anaitwa, lakini alipokuja Yanga iliyokuwa na DONALD NGOMA, AMISE TAMBWE, OBEY CHIRWA, alijikuta anasugua benchi mpaka kujiingiza kwenye ulevi na kudhurumu kipaji chake.

Kipaji cha mchezaji huyu kilipotea kwa sababu ya kufuata fedha za MANJI kwenye timu yenye upinzani mkubwa wa namba au sehemu anayocheza,

Mchezaji mwingine ni Salamba kwa tamaa ya fedha aliingia Simba yenye wachezaji wakubwa kama John Bocco, Emmanuel Okwi, Meddy Kagere matokeo yake Salamba amejikuta anashuka kiwango.

Nina imani Salamba angeendelea kuwa LIPULI kwa umri wake mdogo angecheza mechi nyingi zaidi pia angeendelea kuitwa timu ya TAIFA, mpaka hapo atakapo jiona anaouwezo wa kugombea namba katika timu kubwa.

Bernald Morrison na Deo Kanda walijitambua uwezo wao mdogo kugombea kucheza kikosi cha kwanza ndiyo maana wamekuja Bongo kwenye ligi inayolingana na uwezo wao
 
Kwa hiyo kipimo cha mafanikio ya mchezaji ni kucheza timu ya taifa au kupata fedha? Morrison na Kanda wanacheza timu za taifa?
 
Kwa hiyo kipimo cha mafanikio ya mchezaji ni kucheza timu ya taifa au kupata fedha? Morrison na Kanda wanacheza timu za taifa?
Mchezaji mzuri yeyote anapenda kucheza tena awe kwenye kikosi cha kwanza, ndiyo maana kwenye mikataba ya wachezaji wanaojitambua kipengele cha kuwa kwenye kikosi cha kwanza kinakuwepo.

Mafanikio ya mchezaji ni kusaidia timu yake ya taifa, ndiyo maana kwenye vilabu vikubwa vinapo sajili wachezaji kuchezea timu ya Taifa ni kigezo kimoja wapo.

Deo Kanda yule wa kipindi kile alikuwepo timu ya taifa, sasa hivi sio rahisi kuchezea timu yao ya taifa kutokana na upinzani na vipaji vilivyopo katika nchi yake, labda MAPENDEKEZO YA KOCHA KUMMWITA KWA KUMUAMINI UWEZO WAKE.

MORRISSON kupata nafasi kwenye timu ya taifa ya Ghana ni ngumu sana, sababu nchi hizo zinaamini wachezaji bora wote wanachezea ULAYA, labda anaweza kuitwa kwa mapenzi ya kocha kumuamini,
 
Deo Kanda yule wa kipindi kile alikuwepo timu ya taifa, sasa hivi sio rahisi kuchezea timu yao ya taifa
MORRISSON kupata nafasi kwenye timu ya taifa ya Ghana ni ngumu sana,
Kwa hiyo Deo Kanda na Morrison hawana mafanikio licha ya kujitambua, ila mchezaji wa Lipuli anayechezea timu ya taifa ana mafanikio, au sio?
 
Acha UJUHA na UPUMBAVU (samahani)

Mchezaji mpira hastaafu akiwa na miaka 60. Ana miaka kumi tu ya kujenga maisha yake ya Sasa na baadaye. Hivyo cha kwanza kabisa anachoangalia ni maslahi. Samatta alikuwa na uhakika wa namba Simba lakini akaamua kwenda kupambana Tp Mazembe ambapo kulikuwa na wachezaji wakali sana kina Kabananga akapata namba. Akawa na uhakika wa namba TP MAZEMBE lakini akaamua kwenda Genk ambako hana uhakika wa namba akapambana Leo yupo Aston Villa anakula mamilioni kwa wiki. Kwa akili zako za kijinga ungependa Samatta aozee Simba.

Mchezaji popote ulipo unatakiwa kupambana tu hakuna namna nyingine. Arthur Mello pale Barcelona yupo anapambana ametoka kwenye ufalme wake Gremio kwenda kugombania namba na Vidal na Rakitic..kina Perisic wameenda Bayern kupambana na kina Kingsley Coman. Ramsey kaenda Juve kupambana na kina Pjanic...wapo kina Douglas Costa, cuadrado Juve bado wanang'ang'ana kupambania namba

Tumia akili ndogo tu kuwaambia hao wachezaji wapambane zaidi. Lakini pia washauri vilabu vya soka viwalipe vizuri wachezaji wao muhimu ili wasifikirie kuondoka.
 
we NDIYO MAANDAZI KWELI (samahani)

Kwenye mpira lazima ujue kuna madaraja katika ligi na wachezaji.

Katika ligi kuna nchi ligi zao kubwa, ligi za kati na ligi ndogo, hapo nazungumzia katika ubora wa ligi.

lakini pia kuna wachezaji wa ligi kubwa mf, UK, German, Italy Span etc.
unamzungumzia Samatta mchezaji ambaye anao uwezo wa kupigania namba katika ligi yeyote hapa dunia!!!

lakini kuna wachezaji wa timu ndogo kama vili lipuli, Mbao wachezaji awa wakiwa kwenye timu hizo wanacheza vizuri sana lakini wakija timu zinazotaka matokeo kama simba na yanga hawawezi kuonesha uwezo wao.

kikubwa mchezaji kujitambua yeye ni wadaraja gani??
 
Mshindo msola toka kuwa mshauri wa benchi la ufundi wa simba na kuchezea simba veteran ya morogoro hadi kuwa kiongozi wa yanga.. huku ni kutojitambua.. NUGAZ nae kutoka kundi la ushangiliaji la kidedea la simba hadi kuwa mhamasishaji wa yanga huku pia ni kutojitambua na kuidhulumu nafsi yako
 
Unamtaja Samatta kama ana uwezo wa kupigania namba ligi yoyote duniani na ni kwa sababu tayari yuko ulaya.
Je alipokuwa Africa lion ungeweza kutambua kuwa ana uwezo wa kupigania namba ligi yoyote duniani?
 
 
Unamtaja Samatta kama ana uwezo wa kupigania namba ligi yoyote duniani na ni kwa sababu tayari yuko ulaya.
Je alipokuwa Africa lion ungeweza kutambua kuwa ana uwezo wa kupigania namba ligi yoyote duniani?
Narudi pale pale kujitambua wachezaji na vipaji vyao

Kuna wachezaji wamepewa kipaji na Mungu na wale wanaocheza mpira kwa sababu amefundishwa kucheza mpira na kufanya mazoezi.

Samatta anajitambua anacho kipaji cha kucheza mpira, na kweli yeye mwenye anatambua kipaji na uwezo wake pia yupo tayari kulinda uwezo wake.

Ibrahimu Ajibu Mungu amempa zawadi ya kipaji cha kucheza mpira, watu wa aina ya Ajibu sio wengi hapa Tanzania na duniani pia, lakini kutotambua kipaji chake.

Hii imethibitishwa na walimu kadhaa wa mpira wa miguu.
 
Mfano unajijua wewe ni wa daraja la Kati halafu Simba wameweka milioni 100 mezani na mshahara milioni 5 kwa mwezi utabaki Yanga, mbao au lipuli fc uendelee kupata laki nne kwa mwezi kisa unacheza?
 
Mfano unajijua wewe ni wa daraja la Kati halafu Simba wameweka milioni 100 mezani na mshahara milioni 5 kwa mwezi utabaki Yanga, mbao au lipuli fc uendelee kupata laki nne kwa mwezi kisa unacheza?
Ndiyo hivyo kupanga ni kuchagua unasajiliwa kwaa fedha nyingi, kwenda kukaa benchi, msimu unaofuata anatolewa kwa mkopo NAMUNGO Fc, mara unaenda kuchezea UJENZI Rukwa, mwisho atasajiliwa na CDA ya dodoma kwenda kupandisha timu.

halafu maisha mengine yanaendelea ndani ya NDONDO CUP.
 
Mfano unajijua wewe ni wa daraja la Kati halafu Simba wameweka milioni 100 mezani na mshahara milioni 5 kwa mwezi utabaki Yanga, mbao au lipuli fc uendelee kupata laki nne kwa mwezi kisa unacheza?
Kama Mbaraka Yusuf, alikuwa kijana mwenye kipaji cha hali ya juu, aliwahi kuwa mfungaji bora hapa Tanzania, sasa hivi yupo timu gani vile!!!!!

lazima tukubali kuna mchezaji kwa ajili ya timu kama Kagera Sugar, Mtibwa, Lipuli, mbao etc, hizi timu hazina presha wanachokitaka wao kubaki kwenye ligi.

Simba, yanga, azam hizi ni timu zinazotaka ubingwa na makombe hivyo zinataka ushindi tu, kinyume na hapo wanakufukuza fasta.

pia kuna mchezaji kama Tshishimbi huyu ni mchezaji wa mechi za kama vile Yanga na Simba, Yanga na Azam, hapo utamuona huyu jamaa bonge la mchezaji na umuhumu wake katika kikosi utamuona.

Lakini Tshishimbi kwenye mechi Yanga na Lipuli, JKU huyu jamaa utamchukia haina ya uchezaji wake yaani anakuwa sio msaada kwa timu.

mwisho wa siku wachezaji lazima wajitambue wapi wanafit, watacheza kwa muda mrefu na kuwa na manufaa, maana mpira ni biashara.
 
Mleta mada shida yako unaamini mchezaji akipata nafasi za kucheza nyingi ndiyo kafanikiwa kimaisha. Mpira umebadilika Sana kutoka burudani au kipaji kuwa ajira, mchezaji wa leo yuko kimaslahi ukilinganisha na waliocheza miaka ya 1970s, '80s, 90s ambao walicheza kutetea club zao!

Kipindi hicho haikuwa rahisi mchezaji wa Yanga kumsajili Simba au wa Simba kumsajili Yanga.
Dunia ya Sasa Ni ya fursa, huwezi kubaki unasifiwa kucheza mara nyingi kwenye team huku maslahi duni.

Unapolalamika bila kujua malengo ya wachezaji unakosea, lazima watumie fursa yoyote iliyo mbele yao kuandaa maisha baada ya kuachana na soka ambalo hudumu kwa mda mfupi Sana!
Ajibu na Gadiel walijua yote haya kuwa Simba sc Ina wachezaji wengi wa viwango Bora kuliko walikotoka Yanga, Ila maslahi ndiyo maisha.

Usipende kukosoa maamuzi ya watu katika maisha yao, una nafasi kubwa ya kujikosoa mwenyewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…