DITOPILE WAPILI
JF-Expert Member
- Oct 19, 2015
- 384
- 261
Deo Kanda ni mchezaji aliyetokea TP-Mazembe ya CONGO, kuja kucheza mpira Club ya Simba ya Tanzania.
TP-Mazembe ni moja katika timu tajiri na bora katika bara la Afrika na imekwisha chukua vikombe mara kadhaa vya bara Afrika.
Deo Kanda anaondoka TP Mazembe, akiwa na mshahara mzuri tu, kuja simba kwa mkopo sababu kubwa alikuwa hana nafasi ya kucheza wala kuanza katika kikosi cha kwanza katika Club ya TP-Mazembe, ndiyo maana sasa hivi yupo katika kikosi cha Simba.
Ndani ya Kikosi cha Simba Deo Kanda amekuwa LULU na mtamu kama mcharo, pia kuna tetesi kuwa TP-Mazembe wanamtaka tena Deo Kanda, lakini Deo Kanda hayupo tayari kuondoka Simba anafurahi maisha ya kuwa Simba pamoja ufalme na thamani aliyopewa club ya wekundu hao wamsimbazi.
Ibrahimu Ajibu Mzee wa makorokocho, mguu wa dhahabu majina hayo na sifa aliyapata alipokuwa kapteni wa Timu ya Yanga.
Lakini kutokana na Yanga kuyumba kiuchumi, na ushawishi wa fedha "MO" Ajibu anakwenda kujiunga na Club ya Simba.
Ndani ya Club ya Simba kutokana na wachezaji wanaunda kikosi hicho, Ajibu hana namba ya kucheza hata kwenye kombe la mapinduzi.
Wachezaji wengine waliotoka Club kubwa kuja kucheza ligi yetu ya bongo kwa sababu ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza ni Bernard Morrison raia wa Ghana aliyetokea Afrika ya Kusini timu ya Orlando Pirates.
Sasa hivi Bernard Morrison amekuwa mfalme ndani ya Yanga, huku Gadiel Michael na Beno Kakolanya wanaendelea kukalia mbao katika timu ya Simba.
Kwa akili hizi wachezaji wetu watasugua sana benchi, wanashindwa kutambua kwamba thamani yao inalindwa kwa kucheza mpira, sio kupokea mshahara.
Sipati picha mchezaji wa kutengemewa na club pamoja na timu ya taifa anatoka kwenye timu ambayo anao uhakika wa kuanza kwenye kikosi cha Kwanza na kucheza mechi zaidi ya asilimia 90%, kwenda kwenye timu ambayo hata kwenye wachezaji wa akiba hayumo kabisa.
Haya sasa kwa tamaa ya fedha endelea kusugua bechi, kipaji kinakwisha na muda nao sio rafiki sana.