Watambue Wanachama wa Vyama Mitandaoni

Watambue Wanachama wa Vyama Mitandaoni

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana kumekuwa na kasumba ya kuwafungamanisha wajumbe mitandaoni na vyama vya siasa labda kulingana na maudhui ya mabandiko yao.

Dhana hii kwa hakika ni potofu sana, hasa pale wajumbe husika wanapokuwa hawajijitanabaisha hivyo wazi wazi na kwa IDs zilizokuwa verified.

Itoshe kusema ni kuvikosea sana vyama na viongozi wao, kuwavesha mawazo ya wajumbe wasiojulikana mitandaoni kuwa eti ndiyo misimamo yao rasmi au vyama vyao.

Niazime maneno ya mwanamziki mmoja nguli, "huo ni ushamba!"

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Mkuu hili ni tatizo hata kwenye hoja muhimu za kitaifa watu wanaleta ushabiki wa kijinga kabisa mfano ni hoja ya katiba mpya na kupata haki
Hoja hii ni kuntu, lakini hushambuliwa vikali na wajinga na wapumbavu wachache kama Elitwege , Wakudadavuwa, Bwana Musiba a.k.a Nigrastratatract na lumumba fc wengine.
Siku mama anapoanzisha tena huu mchakato sijui wataficha wapi sura zao
 
Wataanza kuibuliwa watu wa hovyo na kuingizwa bungeni kwa lazima

Mabilioni ya watanzania yako chooni na kwengineko wakati makabrasha ya katiba mpya yanapigwa na vumbi kwenye makabineti.

Tunataka Katiba mpya haiwezekani roho za watu zaidi ya 60Millioni ziamuliwe na mtazamo wa mtu mmoja kuhusu corona na chanjo yake. Haiwezekani. Angalau yule aliyesema tumtegemee Mungu ambaye ndiye muweza wa yote na muumbaji wetu aliye na huruma juu yetu. Maamuzi ya mtu mmoja huku akipigia jicho na kuangalia USD 400M yatatugharimu kama Taifa.
 
Mimi mwanachama wa chadema sitaki katiba mpya

Bila kuwa na verified user ID hujakidhi vigezo:

IMG_20210629_170355_666.jpg

Kujinasibisha wewe na Chadema au viongozi wake kwa msingi wa mada, "huo ni ushamba!"
 
Mabilioni ya watanzania yako chooni na kwengineko wakati makabrasha ya katiba mpya yanapigwa na vumbi kwenye makabineti.

Tunataka Katiba mpya haiwezekani roho za watu zaidi ya 60Millioni ziamuliwe na mtazamo wa mtu mmoja kuhusu corona na chanjo yake. Haiwezekani. Angalau yule aliyesema tumtegemee Mungu ambaye ndiye muweza wa yote na muumbaji wetu aliye na huruma juu yetu. Maamuzi ya mtu mmoja huku akipigia jicho na kuangalia USD 400M yatatugharimu kama Taifa.

Uwepo wa katiba mpya uko mikononi mwetu.

Hatutapewa na mtu kwa utashi wake. Mandela anasema: 'No easy walk to freedom."

Huo ndiyo ulio ukweli mchungu.
 
Safari hii tutaipata vinginevyo CCM watarudia kuweka jezi zao kwenye visalifeti.
 
Mkuu hili ni tatizo hata kwenye hoja muhimu za kitaifa watu wanaleta ushabiki wa kijinga kabisa mfano ni hoja ya katiba mpya na kupata haki
Ccm toka afariki mzee nyerere kambarage haijaweza hatamaramoja kubeba nakufanyia kazi hoja zakwake hizi ngumu kama katiba unaona wanafeli wanaishia njian
 
Mabibi na mabwana kumekuwa na kasumba ya kuwafungamanisha wajumbe mitandaoni na vyama vya siasa labda kulingana na maudhui ya mabandiko yao.

Dhana hii kwa hakika ni potofu sana, hasa pale wajumbe husika wanapokuwa hawajijitanabaisha hivyo wazi wazi na kwa IDs zilizokuwa verified.

Itoshe kusema ni kuvikosea sana vyama na viongozi wao, kuwavesha mawazo ya wajumbe wasiojulikana mitandaoni kuwa eti ndiyo misimamo yao rasmi au vyama vyao.

Niazime maneno ya mwanamziki mmoja nguli, "huo ni ushamba!"

Au nasema uongo ndugu zangu?
Bandiko zuri.

Ubarikiwe.
 
Back
Top Bottom