Watanganyika Hawaipendi Tanganyika Yao?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Mimi ni Mtanzania. Nimezaliwa na kukulia upande wa Tanzania Bara, yaani, Tanganyika.

Nimeshamsikia zaidi ya mtu mmoja akijitambulisha kuwa yeye ni Mzanzibar. Lakini sijawahi kumsikia mtu akijitambulisha kuwa ni Mtanganyika. Mimi binafsi sijawahi kifanya hivyo.

Je! Inawezekana Watanganyika hawaipendi Tanganyika yao kama Wazanzibar wanawanavyoipenda Zanzibar yao?
 
Hao watanganyika wanaojona raha kujiita wazanzibari kwanini wasihamie huko Zanzibar? kwanini wanajitesa bila sababu, au hawana nauli ya boti?
 
Kama hujawahi kumsikia mtu yeyote akijitambulisha Utanganyika wake,basi mimi niwe wa kwanza ,Mimi ni Mtanganyika.
Samahani mkuu, kabla ya leo ulishawi kukutana na mtu anayejiita Mtanganyika?
 

Wengine tukisikia Tanganyika, tunakumbushiwa ukoloni ukoloni vile.
 
Tanganyika ilizikwa tarehe 27-04-1964 kwa presidential decree, na Mtanganyika mwenzetu.
 
Ukweli watanganyika ndio nchi yao inaitwa tanzania. Hata muungano ukivunjika kesho tanganyika itaitwa jamhuri ya tanzania. Hao zanzibar wasiwe na shaka wanaweza kujiita tu wazanzibari maana hawatupunguzii kitu kama hawaitaki tanzania.
 
Baada ya muungano wetu adhimu, kwa nchi mbili za iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kuungana na kuunda nchi moja mpya ya JMT, Tanganyika ilikufa na nafasi yake kuchukuliwa na Tanzania Bara, hivyo Tanganyika haipo, it's no more!, it doesn't exist anymore!. Lakini Zanzibar still does exist, japo sio nchi kama nchi bali ni sehemu ya Tanzania lakini ipo!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…