Adverse Effect
JF-Expert Member
- Oct 8, 2017
- 2,049
- 5,449
Moja kwa moja kwenye mada.
Tukiendelea kukaa kimya na kufumba macho pamoja na kuziba masikio tunajidanganya.
Sakata la Loliondo miaka ya 90 utawala wa Rais Ally Hassa Mwinyi uliwafurusha wamasai na kuwaweka waarabu, tukasema hayatuhusu. Ingawa wapo waliopaza sauti hadi kupoteza maisha. Heshima kwa shujaa Stan Katabalo kwa kutumia kalamu na taaluma yake kufichua uovu.
DP World kupewa bandari ya Dar es Salaam kwa kikundi au genge la kampuni ya Waarabu wa Dubai kwa makubaliano na mikataba isiyo na tija kwa taifa na iliyojaa makando kando mengi. Hapa kidogo niliona watanganyika wakipaza sauti na kupinga ingawa waliishiwa nguvu ikapita hiyo.
Kinachoendelea Ngorongoro ni hakina tofauti na kile kilichofanyka wakati wa Serikali ya Rais Mwinyi.
Watanganyika tujiulize na tutafute majibu, utawala wa Rais Samia anafata nyayo za utawala wa Rais Mwinyi? Sisi watanganyika tunanufaikaje na hao waarabu kwa sasa? Tutakaa kimya mpaka lini kuangalia dhuluma na uonevu wanaofanyiwa wenzetu wamasai?
Wajameni tuamkeni usingizini, wamasai wote ni ndugu zetu na ni marafiki zetu na ndio maana wamasai kila mtu aliyekuwapo mbele yake anaitwa rafiki.
Hatuwezi na kamwe hatutavumilia ukatili na uonevu wanachofanyiwa ndugu zetu na marafiki zetu wa jamii ya Wamasai.
Tuungane na tuwe kitu kimoja kupinga na kukemea uovu na udhalimu pamoja na dhuluma kwa wenzetu.
Rais Samia na serikali yako tunakusihi na tunakutaka uache mara moja kuwaonea na kuwanyanyasa watanganyika wenzetu.
Mwisho ila sijamaliza sisi watanganyika ni wapole na wanyenyekevu ila tusichukuliwe poa.
WAKATI WA UKOMBOZI NI SASA, AMKENI MLIO LALA TUSIENDELEE KUIBIWA.