BICHWA KOMWE -
JF-Expert Member
- Jul 21, 2022
- 6,373
- 16,073
Famchezo nini!! Ukinyukwa kirungu cha ugoko lazima utoe gesi kwa mkupuo.
Historia inaonesha watanganyika wanaogopa matokeo ya maandamano kuliko maandamano yenyewe.
Mwaka 2018, Bwana Mbowe aliitisha maandamano lakini akaambulia patupu. Hakuna mtanganyika aliyejitokeza.
Baadaye dada uchwara wa Taifa naye akaitisha maandamano huku yeye akiwa Ulaya, akaishia kupata aibu na fedheha kutokana na mikwara lukuki aliyoitoa ya kuitisha serikali halafu mwisho wa siku watanganyika wakajificha majumbani mwao.
Licha ya historia kuonesha pia kwamba hatukuwahi kupata madhara ya umwagaji damu yaliyotokana na maandamano, lakini watanganyika wengi wamekuwa waoga kutokana na kupigwa biti tu na maafande. Kumbe mkwara tu unatosha kuwanyausha watanganyika hawa.
Watanganyika hawa ukitaka kuwakonga, itisha kusanyiko la kushabikia mpira. Watamiminika kama sisimizi.
Au itisha fiesta, watakuja kwa mafuriko mpaka nafasi zitapelea.
Ole wako umwambie aandamane kupigania bei ya sukari kushuka, anatoka nduki anaenda kujibanza uvunguni.
Sijui ni ukali wa virungu vya polisi au ni woga tu kurithi? Hii hofu inafikirisha.
MY TAKE: Hili nalo mkalitizame.