Watangazaji 3 redio ya Waziri Kagasheki mbaroni kwa wizi

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Posts
1,769
Reaction score
1,390
Nimepata taatrifa kutoka Bukoba kuwa Wamekamtwa watangazaji wanne wa redi kasibante ya Bukoba Mali ya Kagasheki kwa tuhuma za utapeli,kughushi majina na kuiba kifaa cha kurusha matangazo live mali ya waziri kagasheki.

waliokamatwa ni pamoja na
1.Abela Kamala-Meneja wa redio
2.Emmanuel Mbaule-Meneja wa Vipindi
3.Bw Mutabuzi-Meneja Ufundi

hadi sasa wapo ndani kituo cha polisi bukoba mjini.
 
nimewasiliana na jamaa hapo redioni anadai kuwa waliokamatwa ni abela na mutabuzi,mbaule amelala mbele anasakwa,kwamba eti wakiwa wasimamizi wa redio wameiba fedha na vifaa baada ya kuingia mkurugenzi mpya richard leo akaini wizi huo,

lakini my take hapa ni kuwa hii redio ni ya ccm kufanyia propaganda zake na huyo mbaule alikuwa akitoa matusi kwa lwakatare 2010 hivyo ngoja atoswe na akumbuke ccm hawana shukrani
 
nani kawakamata? hapo mwizi kakamata mwenzake. leta story za huko bukoba. vipi lile kanisa kubwa lilokuwa linajengwa hapo mbele ya pilisi nafikili ni lumuli limeshamalizika?.
 
Kwa hili la kughushi nafikiri watanzania kweli tumekubuhu sana ..duh!
 
Njaa haina shujaa! Baada ya siku si nyingi tutasikia the same saga kwa watangazaji wa Star tv na Radio Free Africa..nasiki mwezi wa tatu sasa watangazaji wa Star tv na RFA hawajalipwa mishahara na Diallo yupo busy na underground movement kutetea tena ubunge wa jimbo la ilemela. Siasa na biashara ni mlenda na chai!
 
nani kawakamata? hapo mwizi kakamata mwenzake. leta story za huko bukoba. vipi lile kanisa kubwa lilokuwa linajengwa hapo mbele ya pilisi nafikili ni lumuli limeshamalizika?.

Jiandae mwezi wa kumi kuhudhuria ufunguzi wa Cathedral na kuhamishwa kwa mwili wa Mha. Raulean Rugambwa hapo Cathedral. .....liko tayari!
 
nani kawakamata? hapo mwizi kakamata mwenzake. leta story za huko bukoba. vipi lile kanisa kubwa lilokuwa linajengwa hapo mbele ya pilisi nafikili ni lumuli limeshamalizika?.

wamekam,atwa na polisi bukoba central,kuhusu jengi ni kuwa litazinduliwa rasmi 6/10/2012(siko bk lakini nina update daily)
 
hadi meneja? hao hawajaiba kuna ishu upande wa pili. N mwanzisha uzi basi jitahidi tupate upande wa pili wa story, usikute hawajaiba bali wamerudisha mali zilikuwa zimeibiwa na mwenye kampuni. lol
 
Duuuuuh hawajawalipa mishahara nini? Maana wafanyakazi kama wana madai wanaweza kukuhujumu ukitoa tamaa ya utajiri wa haraka haraka.
 
Bila shaka kutakuwa na tatizo!

Haiwezekani ikawa unalipwa mshahara mzuri halafu ukawa na mambo ya udowezi.

Mi nafikiri hakika kuna jambo na tutasikiaga tu!
 
Naye hivyo vitu kapata kwa njia ya wizi tu
awaache wenzie kwani nao wanataka wawe kama yeye.
 
Emmanuel Mbaule: amechezea pabaya, kwa level aliyokuwa amefikia (meneja) hakupaswa kufanya hivyo; kwanza anawakwamisha vijana wenzake kupata kipato: OB-Van kachukua na baadhi ya vifaa muhimu kwenye Studio kalamba zikiwemo na pesa tasilimu. Kwakweli inasikitisha sana ila kwa Kagasheki nina imani atamkamata tu na sheria itachukua mkondo wake.
 
tayari Emmanuel Mbaule(meneja Kasibante FM) aliyeiba Vifaa vya Studio/Redio ya Mh.Kagasheki (Kasibante Redio FM ya Mjini Bukoba) amekamatwa na sasa hivi yuko mikononi mwa Polisi kwa mahojiano na upelelezi wa Awali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…