Watangazaji Azam hawajui kiingereza?

Jane Lowassa

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2016
Posts
4,955
Reaction score
9,041
Ni wale wanaohoji makocha baada ya mechi.

Kuna mmoja alikuwa anamhoji kocha wa Simba wa makipa baada ya mechi na JKT. Yaani aibu niliona mimi aisee. Full kujichanganya mfano "what did your players gave you". Mwishoni akashindwa kusema thank you akasema "shukrani"

Ni aibu kwa kweli. Jipigeni msasa kabla mambo hayajawa mabaya sana.
 
😎Lugha inahitaji kuijua,mazoea ya kuitumia kuongea na kuandika,wepesi wa uumbaji maneno na utunduutundu.Usicheke wala usione aibu.Kila lugha ina tabia yake kwa mtumiaji asiye wa asili.
 
Kuna yule msemaji wa club mtangazaji wa Azam ni mkali sana wa lugha yule dogo, simjui jina kaiva kwenye lugha, English imeenea 💯💯💯
 
Elimu, elimu, elimu. BURIANI LOWASSA
 
Hata mie nimeona hili Sana.
Ninachokiona Hawa Jamaa ikitokea wanamhoji kocha wa kibongo maswali ni mengi Sana,sasa ngoja ifike zamu ya gamondi na benchikha ni majanga
Hata mie nimeona ikifika zamu ya gamondi na benchikha Jamaa wanasikitisha Sana. Ni aibu kubwa kwa level za Media kama Azam.
 
Asilimia 75 ya Watangazaji wa mpira wa miguu na wachambuzi hawajui kabisa kiingereza.
1. Kitenge
2. Eddo Kumwembe
4. Baraka Mpenja
5. Nyembela
 
Asilimia 75 ya Watangazaji wa mpira wa miguu na wachambuzi hawajui kabisa kiingereza.
1. Kitenge
2. Eddo Kumwembe
4. Baraka Mpenja
5. Nyembela
Patrick Nyembera yuko vizuri mtoe hapo usimuweke kundi moja na Kitenge aliyezungusha form six pale Al-Haramain
 
Elimu, elimu, elimu. BURIANI LOWASSA
Kumbe kujua Kiingereza ndio Elimu!
China hawajui Kiingereza wametoboa.
Mrusi hajui Kingereza anaRun dunia.
Nenda India, Malaysia nk.
Huu ujinga upo Afrika tu kwa wajinga wachache tambua Kiingereza ni Utumwa, Kataa kuwa mtumwa, KUZA KISWAHILI, KOMAA NA KISWAHILI IWE BIDHAA YA KUUZWA DUNIA NZIMA Watakuja kujifunza tuu.
Nyie mnaopenda showoff endeleeni na Viinglish vyenu na utumwa wenu vichwani.
 
Mimi binafsi nishajiuliza muda mrefu, wengi wao ngeli huwa inawapa shida.

Tatizo la kwanza walilonalo ni kutumia sentensi ndeeeefu kuuliza kitu kidogo na cha kawaida. Wangekuwa wanakuwa short and precise.

Ni bora wangekuwa wanajiandalia short written questions zisizokuwa na poor grammertical errors ili waulize maswali yenye utimamu.

Ofisi yao ione namna bora ya kuwanoa kwenye kipengele cha lugha.

Mwisho Azama waajiri pia watanzania wengine ambao wako vizuri kwenye ngeli ili wawe wanatangaza mechi kwa kimombo.
 
China na Russia wamefanya lugha zao za tauafa kuwa na uzito kwa kuwa nchi zenyewe zina uchumi imara.

Sasa Tz na Kiswahili chetu na uchumi wetu wa kutegemea misaada unadhani nani atakayetujali.??
Kubali kataa kujua English kwa dunia ya leo hasa kwa nchi masikini ni kipaumbele sana.
 
Tanzania hakuna mtangazaji yeyote anaejua English sio wa Azam tu.
 
Azam media bila kuvaa kibaragashia kazi hupati, watangazaji wao wamekaa kiswahili Swahili mda wote kuitana sheikh sheikh, waajiri wafanyakazi Kwa kutoangalia kibaragashia
 
Shukuran ni kiarabu na yule kocha anakijua hivyo hakuna shida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…