PAGAN
JF-Expert Member
- Aug 19, 2014
- 12,181
- 20,148
Na kamwe usingejua kama ni Magazeti bila ya Wewe pia kuwa Msomaji wa hayo hayo Magazeti yangu. Na Uandishi wangu huu huu wa Kimagazeti ndiyo unafanywa niwe ' Followed ' na Watu zaidi ya 47 humu lakini pia ID yangu ikiwa ni miongoni mwa ID's ambazo zinaongozwa Kupitiwa na Kufuatiliwa kila siku. Na kama haitoshi ni Uandishi wangu huu huu wa Kimagazeti ndiyo unafanya niweze kuleta ' impact ' hasa yale maeneo ambayo huwa nayagusia katika Mada zangu mbalimbali. Na pia ni Uandishi wangu huu huu wa Kimagazeti ndiyo unafanya hadi Mitandao na Redio mbalimbali hapa nchini Kupenda kutumia ' Maandiko ' yangu ili kuwavutia zaidi ' walaji ' wao. Na mwisho kabisa ni Uandishi wangu huu huu wa Kimagazeti wa GENTAMYCINE ndiyo umepelekea hadi Taasisi muhimu na Ofisi ya anayekuongoza hapa Tanzania wawe ' wanaikodolea ' hii ID kila uchao ili kuona naandika nini na najivunia kuwa kati ya mambo ambayo huwa nayaandika hapa basi 75% yake huwa yanazingatiwa na kufanyiwa Kazi.
Chuki zenu Kwangu ndizo zinanifanya hadi muwavutie Watu wengine hapa kupenda kunifuatili hivyo nakuomba Wewe na ' Wapumbavu ' wenzio ambao mnachukizwa na kukerwa na hii ID msiache Kunichukia kwani ndiyo ' mnanipaisha ' zaidi hadi kuwa na mvuto wa Kipekee unaohitimishwa na ' Signature ' yangu isemayo ' Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer '.
Nasubiri sasa kusikia na Wewe ambaye huandiki ' Magazeti ' una ' impact ' gani katika uwepo wako hapa kama Member ili nami na wengine waweze Kuupima ' vividly '. Na hamtoweza Kunivunja moyo wala Kunirudisha nyuma kwa lolote na kama bado nipo Hai hivi nitaendelea kuwepo hapa Jamvini 24/7 na kuandika mambo mbalimbali, kufanya chambuzi zangu za Kiuandishi na za Kimawazo na kutoa maoni mbalimbali ya Kimaarifa katika yale ambayo nayajua na nayaamini.
Mwisho kabisa Utafiti mdogo ambao nimeshaufanya humu na kuna siku nilishasema na leo naurudia tena ni kwamba 95% ya wale Members wanaojifanya ' Kunichukia ' au ' Kukereka ' nami ' actually ' ndiyo Members ambao ' wananikubali ' na hawaachi kunifuatilia hapa kila Uchao kujua nimeandika nini na kuna wengine japo mkiwa hapa mnajifanya Kunichukia ila mawazo na maono yangu huwa mnayachukua na kuyatumia sana huko mlipo na kuonekana mpo vizuri wakati kumbe mmemchungulia ' Mwanamume ' humu.
Na siku zote Uandishi wangu hapa Jamvini ukiwa ' Mpumbavu ' kama ulivyo pamoja na hao Wenzako hutoweza Kuujua na Kuuelewa ila mwenyewe najua natumia mbinu gani na ipi ya Kiuandishi ili niweze Kufikisha ujumbe ' Kusudiwa ' na kuna muda huwa naweka ' Upuuzi ' fulani ambao ndani yake kuna Ujumbe na nashukuru Watu ' Werevu ' huwa wanakuwa wepesi kunielewa na tunaenda sawa. Najua ' Natural Charm ' yangu ndiyo inawasumbueni na kuwatesa ila nadhani kama ni wa kumpelekea hizo ' Chuki ' zenu basi mzielekeze kwa Mwenyezi Mungu aliyeniumba na ' Kunibariki ' hivi nilivyo na kuwaacheni nyie hivyo mlivyo.
Usisahau pia ' Kuwafowadia ' ujumbe huu adhimu kabisa ' Wapumbavu ' wenzio wote na wale wataojitokeza huko mbeleni.
Nimemaliza.
Acha umbwiga.