Watangazaji wa michezo vichwa, ovyo

Watangazaji wa michezo vichwa, ovyo

Ulipomtaja tu Maulid Kitenge ' fasta ' sana nikamkumbuka ' Mwarabu ' mmoja hivi Merey Balbhabou Mzee wa TIOT. Naomba niishie hapa tafadhali.
Gafla nimeikumbuka moro united,vipi jamaa alikuwa na uhusiano na mau?
 
Gafla nimeikumbuka moro united,vipi jamaa alikuwa na uhusiano na mau?

Naona unachokitafuta sasa ni majibu ya Shombo kutoka Kwangu kisha uanze Kunilaumu. Endelea ' Kuitibua ' Mizimu yangu nikushushie sasa hivi ICBM ukalale nalo vizuri. Kuna Watu mnakera ' to the extent kabisa Swine '.
 
Kumchukia mtu ni dhambi : Ila upande wangu huyu dogo anajiita Nicasius Agwanda "Kotinyo" ni mchambuzi wa hovyo Tz nzima.
Matamshi anavyoyatoa hunifanya nisisikilize kipindi na mbaya zaidi anapenda kudandia uchambuzi pindi mwenzake anapoongea.

Ni mchambuzi wa SportsXtra kitengo cha Basketi (NBA) ila nashangaa anaweza wanyamazisha wakina shafii (Soka) nao wanamstahi wakati anaongea pumba tupu.
 
Sawa mkuu niwie radhi mimi.
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Sipendi wale wanaobana visauti kama yule Tom Chilala. Bado nasema shafii, Edgar, Jeff, Ambangile, 'ticha', Sued Mwinyi na Luambano ni watangazaji vichwa!!! Kitenge na Waarabu! Mmmmh Du! Kumbeee!!!!!
 
Kumchukia mtu ni dhambi : Ila upande wangu huyu dogo anajiita Nicasius Agwanda "Kotinyo" ni mchambuzi wa hovyo Tz nzima.
Matamshi anavyoyatoa hunifanya nisisikilize kipindi na mbaya zaidi anapenda kudandia uchambuzi pindi mwenzake anapoongea.

Ni mchambuzi wa SportsXtra kitengo cha Basketi (NBA) ila nashangaa anaweza wanyamazisha wakina shafii (Soka) nao wanamstahi wakati anaongea pumba tupu.

Nakubaliana na wewe. Ana kijisauti cha hovyo na hujifanya mjuaji sana. Huwa anaharibu sana ladha ya sports extra ya clouds fm!
 
Kama post yako shaffih yupo basi hakuna ulichoandika ni rubbish

Mimi sioni tatizo la Shafii. Anyway watu tunatofautiana mawazo. Hapa ni mahali pa kuelimishana guys. Humohumo kwenye rubbish unaweza kuokota almasi!!
 
Mimi sioni tatizo la Shafii. Anyway watu tunatofautiana mawazo. Hapa ni mahali pa kuelimishana guys. Humohumo kwenye rubbish unaweza kuokota almasi!!
Shafih ni mweupe sana yule jamaa hajui lolote yupo pale cmg kiujanja janja tu toka enzi hizo,,

Narudia tena shafih ni shabiki tu wa mpira kama sisi ila kwenye uchambuzi na tactics za mpira ni mweupe sana,zaidi ya kusoma historia na statistics ambazo hata wew unaweza zipata hama la ziada
 
Sawa ni maoni yako
 
Tigana lukinja anajua kuchambua maana mpira kaucheza yupo EATV ,jamaa anajua halafu hapewi airtime kama hao wabwatukaji kina kitenge
 
Unapozungumzia watangazaji bora wa michezo hivi sasa nchini hutaacha hata kidogo kulitaja jina la Shafii Dauda wa clouds fm.

Ni mtangazaji makini, ametulia, yuko composed and he knows all there is to know about michezo.

Hana mimbwembwe ya ajabu ajabu na ana uelewa mpana wa mambo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa hata katika kada zingine.

Ana brain nzuri, hana papara na ni sensible analyst kwa kweli.

Mwingine kichwa ni Alex Luambano. Ni mweledi sana na anafanya kazi yake kwa umakini mkubwa.

Si mtu wa kukurupuka kama baadhi ya watangazaji. Ana uelewa wa mambo mengi pia sio kama watangazaji wengine ukiwauliza Brexit ni nini utasikia_ mimi mtangazaji wa michezo! Alex nae ni moja ya watangazaji makini kabisa hapa nchini kwa sasa.

Issa Maeda ana uelewa mpana pia na yuko professionally fit. Anajua sana ku interact na wenzake. Hawa wanafanya kipindi cha sports extra ya clouds fm kiwe worthy kukisikiza.

Mtangazaji mwingine mzuri na bora sana wa michezo ni yule wanamwita 'ticha' ( somebody Kinja nadhani) wa EAST AFRICAN RADIO. Ana brain kali sana. Aaaah... He is such a professional dude....

Ni mtaalamu, yuko makini na siku zote anafafanua mambo logically. Unajua utalaamu wa michezo sio kumjua Messi au Ronaldo tu. Ni pamoja na uelewa mpana wa dunia kihistoria, jiografia, siasa, utamaduni na hata uchumi.

Watangazaji vijana learn from this guy. Mtapata madini kedekede lakini mkijifanya wajuaji saana mtaishia kuwa half baked presenters for good!

Watangazaji wengine weledi bila wasiwasi ni pamoja na mkongwe Sued Mwinyi wa tbc, Salum Msabaha_ dogo wa Radio one, Ambangile George_dogo wa Magic fm ( huyu nae ni mtaalamu sana), Omar Katanga wa Azam na Oscar Oscar wa EFM pamoja na kaka yao Maestro ambaye ni mtaalamu kweli lakini nafikiri anaremba mno.

Watangazaji wa michezo wababaishaji na wenye mbwembwe za kitoto ni pamoja na Masare wa Radio one na 'mentor' wake Maulid Kitenge wa EFM. Too much unnecessary ego@ kubana sauti.

Wababaishaji wengine ni Enock Bwigane na Jesse John wa tbc pamoja na dada yao Jane John.

Wale wa sibuka fm nao ni washambashamba fulani hivi. Too much ubabaishaji.
Tom Chilala naye anaharibu sana anaporeemba sauti.
Kilumanga wa Magic fm nae ni bonge la kilaza. The way anachambua mambo hata hayo ya michezo tu, unajua kabisa huyu hamna kitu.
Ni kanjanja fulani hivi. Hapo hujamleta kwenye jiografia. Hachelewi kukwambia Venezuela imepakana na Morocco kwa upande wa kaskazini!! Au Monaco iko karibu na Canada!

dah....teh teh teh teh...kwa kweli nimecheka sana tu..
 
Kuna dogo mmoja clouds anaitwa kotinyo hajafikia viwango vya kuchambua soka kabisa anaharibu kipindi!!....
 
Back
Top Bottom