Watangazaji wengi wa radio hawajui kingereza

Sijakataa kama wapo mkuu...nawasikia sana huko BBC, VOA..kama hujui kiingereza utafanyaje kazi BBC au VOA?..
Unapoteza nguvu zako kubishana na redio, mkuu. Idhaa yenyewe RTD
 
Mkuu unataka mpaka mzungu akuambie kuwa Tanzania ni Masikini ndipo ukubali ?!
Umasikini wa Tanzania mbona uko uchi tu Mkuu..kwani we unaishi Tanzania ipi ndugu yangu!

Tanzania sio maskini, Maskini ni fikra zenu zilizoshindwa kutambua kiongozi yupi bora wa kusimamia rasilimali zenu...! Tanzania ina migodi ya kutosha tu, mito, milima na mengine mengi tu afu bado unasema Tanzania maskini! Huoni kwamba Tanzania sio maskini ila akili za Watanzania ukiwemo wewe ni za kimaskini?
 
zungumza hali halisi iliyopo ukizungumzia nini kinapaswa kufanyika bado hujaondoa ukweli uliopo wa hali ya umasikini.
bila shaka nawewe pia ni mtanzania...hivyo akili za kimasikini nawe zinakuhusu.
 
Huwa nawasikia. Kwa kiswahili kizuri (si fasaha) hawajambo. Tatizo huja pale wanapotamka maneno ya kingereza, ni aibu. Nashauri waajiri wawe wanatilia maanani hii lugha pia maana hao watangazaji wanaaibisha taaluma zao.

Umesema vyema ingawa naona kama kuna watu ama hawakukuelewa ama wanataka kutetea wasichoelewa. Kwa mwanahabari wa Kitanzania kujua kiswahili fasaha na kiingereza cha uhakika ni sharti; si sifa za ziada. Kiswahili ndiyo lugha yetu rasmi ya mawasiliano na lazima tuimiliki kikamilifu. Kiingereza ndiyo lugha tuliyoachiwa na mkoloni wetu na ndio mlango wetu mkuu wa mawasiliano na wenzetu duniani. Ukitaka kuhabarika na matukio na midahalo inayoendelea ulimwenguni bila kukimanya kiingereza ipasavyo utaishiwa kupokea simulizi (za pili) hata zisizo na uhalisia. Kwa mwanahabari unayetutafutia habari za ulimwengu ni shurti uwe na uwezo wa kuzipata katika vyanzo vya awali.

Watanzania tunayo bahati kwamba kiingereza ndiyo lugha inayoongoza kwa mawasiliano duniani; hatuhitaji sana kujua nyingine kama wenzetu wasiokuwa na misingi ya kiingereza kwenye nchi zao. Katika mashirika ya kimataifa, watu waliotawaliwa na Wafaransa, Wareno, Wahispania, Waarabu, n.k. pamoja na kujua lugha zao za nyumbani na za wakoloni wao inabidi wajifunze kiingereza kwa taabu ukubwani ili wakubalike, wakati kwa Watanzania, kiingereza tu chatosha. Ukiongeza lugha nyingine inaitwa "added advantage".

Kinachonitibua sana kwetu sisi Watanzania ni hulka ninayoiona ya wengi kukipenda sana kiingereza huku tukipiga chenga juhudi za kukimanya vizuri kwa visingizio vilivyopitwa na wakati kwamba "sio lugha yetu". Halafu unakuta watu wanaosema hivyo ukianza kuongea nao kiswahili kazi ni kuingiza maneno ya kiingereza na lafudhi za Kiingereza/Kimarekani bila mpangilio kiasi cha hata kuharibu kabisa mawasiliano yenu ya kiswahili. Ukiwabana muongee basi hicho kiingereza ndio taabu kabisa hamuelewani. Ni aina fulani ya "ushamba".

Ndio maana majirani zetu Kenya sasa wanatambulika rasmi kama mabalozi wa kiswahili huko nje kuliko sisi. Tuache mikanganyiko isiyo ya lazima; tuimarishe kiswahili na tujitahidi kukijua kiingereza ili tuweze hata kuwafundisha wengine kiswahili fasaha badala ya kuwaacha Wakenya waendelee kueneza kiswahili chao duni (cha kikabila) ulimwenguni.
 
Mkuu nashukuru kwa hoja yako mwanana. Sasa hawa wapingaji wakija tena na kuanza kukosoa ulichoandika hapa basi huo si ubishi bali ugonjwa. Kimantiki tunawiwa kuijua hii lugha ya kigeni japo kwa ufasaha wa kuielewa na kutamka kwani tunahiaji mengi sana toka huko duniani. Na lugha ya dunia ni kingereza. sasa wanapotokea watu na kusema kujua kingereza ni ushamba na si kitendo cha kizalendo inabidi tuwashangae kwa dhati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…