Watangazaji wengi wa Television na Radio hapa Tanzania wanagangamala sana utafikiri wanakula cement, na wanatumia sauti zisizo zao (artificial)

Emily Lazarus wa Radio One kabobea kwenye kukosea majina. Kila habari lazima akosee jina Mfano kila siku anatamka "Joe Biden" kama inavyoandikwa badala ya "Jo Baiden". Sasa sijui "Peter" atatamka kama inavyoandikwa badala ya kusema "Piter"? Huwa hafanyi utafiti wa namna ya kutamka majina yalioko kwenye habari kabla hajasoma na haangalii habari za nje.
 
Yaani kuna kitu kinanikera mno kuangalia stesheni nyingi za TV Tanzania. Ni kwamba watangazaji wengi sana wa TV, wanawake kwa wanaume, wanapofanya matangazo wanakuwa wamengangamala utafikiri wanaishi kwa kula cement. Unakuta mwili umejikaza hawako natural kabisa, wako very conscious kwamba wanaangaliwa.

Halafu kitu kingine kinaniudhi sana ni karibu Watangazaji 95% wa TV na Radio Tanzania wanabadilisha sauti zao. Na wengi wanaongea kwa kusita sita (kwa pause) wakifikiri ndio inapendezesha kutangaza. Kwa nini lakini? Kwa mfano kuna dada mmoja anatabiri hali ya hewa TVT huwa nikimwona tu nabadilisha channel, ananiudhi mno kujibadilisha sauti na kujifanya anaongea kwa pause.

Kuna wakati Mtangazaji nguli Tanzania, Charles Hilary, alisema wanaongea "kizunguzungu" dada mmoja alipozidisha mno kuongea kwa pause. Charles alimuuliza kama alikuwa ameishi nje ya Tanzania muda mrefu kutokana na lafidhi yake, na huyu dada akasema hapana, ni mazoezi tu. Ndipo Charles akashangaa kwamba ni mazoezi ya kuongea kizunguzungu?

Kwa nini msiwe natural katika kukaa na kuongea? Hivi hakuna mafunzo mnapewa? KUna wengine wanadhani wakiongelea puani ndio Kiswahili chao kinaonekana cha kisomi, ovyo kabisa. Nani aliwaambia kubadili sauti zenu hizo na kuongea kwa pause kunapendezesha utangazaji? Mnakera mno na mnaharibu lafidhi ya Kiswahili. Acheni ulimbukeni. Hamuoni CNN, BBC Skynews wanavyoongea? U-artificial wa nini kwenye sauti zenu? Nani aliwaambia mkiongea naturally hampendezeshi matangazo?
Kuna kitu umesema. Ni cha maana sana. Watangazaji karibu wote wa Bongo, iwe TV iwe Radio au haya ma TV online yaliyoibuka kama mchicha... hawatumii sauti zao za asili. Kifupi huwezi kuwatofautisha.
 
Utangazaji ni kurelax siyo unatoa meno machafu mbele ya mic huku shingo ikitoa mishipa kama miguu ya mbung'o.

Mfano yule anayetangaza magazeti kwa mbwembwe huku akiongea kama anafokeana na mpwa wake.
Kitenge anatumia nguvu sana.
Na kuna wale watangazaji wa vipindi vya bongfleva sauti zao wote kutoka radio tofaut hufanana.
 
Emily Lazarus wa Radio One kabobea kwenye kukosea majina. Kila habari lazima akosee jina Mfano kila siku anatamka "Joe Biden" kama inavyoandikwa badala ya "Jo Baiden". Sasa sijui "Peter" atatamka kama inavyoandikwa badala ya kusema "Piter"? Huwa hafanyi utafiti wa namna ya kutamka majina yalioko kwenye habari kabla hajasoma na haangalii habari za nje.
Ila jamaa ana sauti nzuri sana kwenye habari makosa madogo madogo yanamshusha.

Anaitwa Emilius Lazaro.
 
Ana sauti nzuri sana ila kutofuatlia taarifa za habari za nje na kujifunza namna ya kutamka majina ya watu na miji kutamfelisha.
 
Alikuwa Mwl wangu nyakati fulani jamaa anajua anajitahidi kiasi chake japo makosa yake ni ya wazi.
 
Kumbe na we ushamshtukia? Mara nyingi anachemsha kwenye majina sema nimekumbuka mfano huu mmoja.
Na mtiririko wa usomaji wa habari kuna muda anaenda spidi isiyo kawaida katika usomaji.

Mtangazaji pekee ninaemhusudu ni Ahmed Ally wa Azam Media jamaa anajua sana kufanya kazi pia anajua kutangaza kwa mtiririko mzuri.
 
Yaani kuna kitu kinanikera mno kuangalia stesheni nyingi za TV Tanzania. Ni kwamba watangazaji wengi sana wa TV, wanawake kwa wanaume, wanapofanya matangazo wanakuwa wamengangamala utafikiri wanaishi kwa kula cement. Unakuta mwili umejikaza hawako natural kabisa, wako very conscious kwamba wanaangaliwa.

Halafu kitu kingine kinaniudhi sana ni karibu Watangazaji 95% wa TV na Radio Tanzania wanabadilisha sauti zao. Na wengi wanaongea kwa kusita sita (kwa pause) wakifikiri ndio inapendezesha kutangaza. Kwa nini lakini? Kwa mfano kuna dada mmoja anatabiri hali ya hewa TVT huwa nikimwona tu nabadilisha channel, ananiudhi mno kujibadilisha sauti na kujifanya anaongea kwa pause.

Kuna wakati Mtangazaji nguli Tanzania, Charles Hilary, alisema wanaongea "kizunguzungu" dada mmoja alipozidisha mno kuongea kwa pause. Charles alimuuliza kama alikuwa ameishi nje ya Tanzania muda mrefu kutokana na lafidhi yake, na huyu dada akasema hapana, ni mazoezi tu. Ndipo Charles akashangaa kwamba ni mazoezi ya kuongea kizunguzungu?

Kwa nini msiwe natural katika kukaa na kuongea? Hivi hakuna mafunzo mnapewa? KUna wengine wanadhani wakiongelea puani ndio Kiswahili chao kinaonekana cha kisomi, ovyo kabisa. Nani aliwaambia kubadili sauti zenu hizo na kuongea kwa pause kunapendezesha utangazaji? Mnakera mno na mnaharibu lafidhi ya Kiswahili. Acheni ulimbukeni. Hamuoni CNN, BBC Skynews wanavyoongea? U-artificial wa nini kwenye sauti zenu? Nani aliwaambia mkiongea naturally hampendezeshi matangazo?
Sasa mkuu unataka nitangazee na kiswahili changu kile cha chattle kweli kabsa. 'Hiiiiiii heno nene bhanghosha...'

Sent using myLG leon
 
Ningependa kumwita Pascal Mayalla humu atoe neno. Haya madoido enzi zile aliyaanza Ben Kiko wa Dodoma (Benedicto KIkoroma nadhani). Mimi nataka nikimsikia Pascal Mayala anaongea mtaani na redioni sipaswi nione kuwa ni watu wawili tofauti. Christiane Amanpour wa CNN ni yule yule nyumbani na akiwa kazini CNN
Lini ulimtembelea Christine Amanpour nyumbani?
 
Unamsema kitenge au samsa sali?

Sent using myLG leon
Huyo huyo Kitenge. Kaona usomaji wa magazeti lazima ufoke na kelele za kujirudiarudia kama anaongea na viziwi.

Zembwela akiwa EA Radio alikuwa anafanya kazi kwa utulivu sana hata David Rwenyagira ila combination yao na Kitenge watakuja kutoka studio taya zimetanuka.
 
Kuna uyu wa redio one Simon Kabendera ni kituko kwa kweli

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Back
Top Bottom