Watangazaji wetu kwanini hamjifunzi majina/maneno fulani yanatamkwaje?

Hayo maneno ya maeneo ya ulaya na ugaibuni sio issue sana kwana hata wazungu wenyewe wakija kwetu maeneo yetu yanawashinda kutamka kinachoniudhi ni wale wanaoshindwa kutofautisha kati ya herufi L na R kwenye magari mathalani atatamka magali
Hiyo mizungu si ndio imetuletea Bagamoyo badala ya bwagamoyo na dodoma badala ya idodomiya? Rufiji badala ya Rupwiy
 
Majina mengine unajifunza kwa kusikiliza wenye majina yao. Mfano Hughes inatamkwa Hyuz sasa utasikia mtangazaji anatamka hugiz/hagiz/hagez
Prondo hil ni tatizo kubwa sana sana. Nadhani wale watangazi walio kuwa na uwezo wa kutamka maneno au majina yawe ya watu au Mimi vitongozi nk walisha staafu au hawapo tena ktk tasnia. Ni aibu sana kuna baadhi ya maneno ni very common lakini MTU analitamka tofauti halafu ni mtangazi au msoma taarifa ya habari.
Sasa hapa sijaweka wale ndugu zangu wanao replace 'r' na 'l' yaani inabadilisha kabisa maana ya sentensi.
Hili linawahusu hata viongozi kwwnye hotuba zao. Yaani kifupi ni majanga.
Lakini hata ni matunda ya sisi wabongo wengi hatuna kawaida ya kusoma vitabu. Sasa hizi vocabulary utajifunza vipi wakati hatusomi vitabu vya hadithi au vya kujiendeleza?!!!
 

Huwa wanakera sana, haswa watangazaji wa michezo, inaonekana wengi shule sio nzuri ni kuongea ongea tu. Hata analysis ya mpira hawajui, sasa shida ni pale wanapotaka waaminike kwa kuingiza English ya ajabu.
 
R na L ni janga. Mfano Liver na River mwenye tatizo la L na R hapa kumuelewa shida sana
 
Mkuu nisaidie jina hili la mchezaji wa zamani wa Uholanzi (Nedherlands) linatamkwa vp? Ni Clarence Seedorf
 
Au SWANSEA wanaitamka kama ilivyo.
Badala ya "Swanzi" kama sijakosea pia
 

Ata wewe ukiandikia baadhi ya maneno hutaweza kuyasema/kuyasoma kifasaha.
 
Au SWANSEA wanaitamka kama ilivyo.
Badala ya "Swanzi" kama sijakosea pia
Ha ha ha ha hio ndugu zetu wanatamka kama ilivyoandikwa Kiswahili....its Swan-Sea
 
Kuna siku nimesikiliza kipindi cha michezo asubuhi km sikokei ni redio free africa au kiss fm
Halo yani utafikiri mchambuzi hajawahi kutizama mpira wala hawafahamu wachezaji
 
Ata wewe ukiandikia baadhi ya maneno hutaweza kuyasema/kuyasoma kifasaha.
Ningekuwa mwandishi wa habari au mtangazaji ningejitahidi nitamke kama inavyotakiwa. Kama wewe hapo mzungu akuite Ulaimbo, sio sawa.
 
Ndugu yangu nilisikia siku moja jina la kocha wa Man U likitamkwa redioni, nusura nijifiche uvunguni. Pamoja na kwamba linaonekana gumu lakini huwa linatajwa tajwa na linatamkwa kiurahisi tu "Sosha". Siku hiyo lilitamkwa "soskajei" kitu kama hicho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…