WATANI SIMBA SC HONGERENI

msolopaganzi1954

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2018
Posts
763
Reaction score
379
....Napenda kuandika juu ya watani zangu Simba SC na Kuwapa Hongera juu ya Ubora na Uwezo mkubwa Walionao na Kufanikiwa kuwapa Mzigo wa Kutosha Mbambane wa Eswitini.......Ukweli usiopingika Simba Wana muunganiko Mzuri Sana (Chemistry)
.....Nawapa Hongera Sana juu Scouting yao ya Wachezaji,
Hapa Yanga Tumezidiwa Sana, Najuha Hapa Ndo yale mambo ya 10% Yanapochukua Nafasi.
 
Asante mtani.
Hata Yanga wana timu bora na yenye muunganiko mzuri.
Tofauti yao na Simba sc ni kuwa Simba sc kwa sasa ni Kampuni na Yanga bado ni timu ya wanachama.
 
Huu uzi umekaa kirafiki zaidi, naomba wanasimba wenzangu tusiwapige vijembe watani zetu kupitia uzi huu. Tuwatie moyo na kuwapongeza pia kwa sababu wao ndo vinara wa ligi yetu kwa sasa...HONGERA MTANI!!
 
Simba naomba waingie makundi iwe champions au confederation..wakirudi kwenye TPL tumewapita points 30 ...vibabu vyao haviwezi kucheza mechi 4 ndani ya siku 12..mwezi wa tatu tunatangaza ubingwa
 
Hiki unachosema ni kweli na hata sisi Wanayanga tunajua fika Simba ikipata mafanikio huko nje ni taifa kiujumla litapata sifa
Ila kwa kuwa sisi ni wazee wa utani wa kubeza hata pasipostahili tutaendelea kuiombea mema Nkana Fc.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…