Watani zangu wakaguru.

Watani zangu wakaguru.

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2010
Posts
7,956
Reaction score
5,149
Siku moja nilikwenda Gairo kununua mahindi.Kwa kuwa ulikuwa ni msimu wa mavuno nilikosa nafasi katika nyumba za wageni ila nilibahatika kukaribishwa na mwenyeji mmoja nyumbani kwake nijipumzishe usiku huo.Kesho yake asubuhi nilipoamka nikatoka na mswaki nje nikawa ninajipigia mswaki wangu taratibu.Kugeuka nyuma ninamuona mwenyeji wangu amenisimamia nyuma yangu,mimi nikaendelea na mswaki huku nukijiuliza jamaa vipi mbona amenisimamia na hasemi chochote?Mwisho uvumilivu ukanishinda nikamuuliza kulikoni bwana?Naye bila hiyana akanijibu towela nise chitowele(tumia nasi tutumie)akimaanisha mswaki!!!!
 
Back
Top Bottom