Watani zangu wasukuma hebu punguzeni matumizi ya vyakula, mnaharibu

exalioth

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2016
Posts
2,395
Reaction score
4,152
Mnajifanya wajuaji kumbe mnaharibu

Wakuu habari zenu leo nitaongelea hawa watani zangu wasukuma japo mimi ni mkazi wa morogoro, juzi juzi tulikua kijijini kwao na rafikiangu kwakweli tulipokelewa vizuri familia nzima ilikua na furaha ni familia yenye watu wengi tulionekana kua wageni kweli kweli niliona jogoo wawili wakubwa wamefungwa kamba

Badae rafikiangu alinitembeza kwenye mashamba yao hadi kwenye mbuga za mipunga jioni saa1 tulirudi nyumbani nikiwa nauchovu nikapewa maji ya kuoga saa2:30 msosi ulikua tayari na nilikua na njaa kinoma tulikua tumekaa pembeni kidogo na mwenzangu tukiwa tunachezea simu kupoteza mda alikuja dada mmoja akatukaribisha tukale,

Wasukuma wanadestuli ya kula kwa pamoja wanaume peke yao na wanawake nawao pia upande wao, upande wetu wanaume zilikuja sahani mbili za ugali kubwa na bakuli zilizo jaa nyama na maziwa mgando kwa pembeni, tukala navile mimi navoyapenda maziwa mgando nilikula sana, sasa mimi hapo mawazo yangu yalinituma nimalizie nyama niliokua nmeshikilia mkononi nitoshe

chakushangaza walikuja wadada watatu kutoka kule kwenye upande wa wanawake wakachukua vyombo vyote[emoji38][emoji38][emoji38] badae walikuja kiupya na sinia zilizo jaa nundu za ubwabwa(ubweche) na mabakuli makubwa yaliyojaa nyama za kutosha na soda moja moja kila mtu dah nilibaki naangalia tu maana mwanzo nlikua nmefukia vyakutosha rafikiangu akaniambia mbona umepoa tuendelee[emoji38][emoji38] niliutamani ubweche niligusagusa rakini sikua na namna, noma sana

Wasukuma nawapongeza mnamapokezi mazuri kwa wageni ila kwenye chakula hua mnaharibu maana najua chakula kilichobaki ni kingi mno isitoshe na asubuhi tulipikiwa chakula kingine nundu za ubweche.

=Exalioth
 
We mzembe kweli
 
Na bado ungekoma kama ungeendelea kukaa angalau wiki,,

Kuna uji wa asubuhi unaitwa nyuka.
Alafu baada ya uji unaletewa mahindi ya kuchemsha na
viazi vya kuchemsha"manumbu"na mihogo"mbute"

Tunawafundisha kula watoto wetu wafupi ili mrefuke,
 
Si ajabu niliwai fika ukerewe miaka iyo ..yaani asubuhi ililetwa ugali ya muhogo na supu ya nyama ile nyama ilikuwa siyo ya kawaida ,then baada ya hapo ndio tukapata chai na ratiba zingine kuendelea

Ni desturi waliojijengea kula na ni nzuri yafaa kuiga (sio kishindia chips)
 
Kula chakula cha kutosha na kushiba ndio Jadi ya usukumani
 
Mkuu mi wasukuma nawapa bigup yaani nilishinda kama mpila nachezwa huko huku mara danadana
 
Hatuamini kama ‘ubweche’ ni chakula cha kushiba bali ni ladha tu, so huwa ni muhimu kuanza na ugali kama stata kisha ubweche hasa siku za ugeni au tukio..... halafu usiseme ni uharibifu kwa maana hakuna namna yoyote ile kuwa ubweche unatupwa.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Na bado ungekoma kama ungeendelea kukaa angalau wiki,,

Kuna uji wa asubuhi unaitwa nyuka.
Alafu baada ya uji unaletewa mahindi ya kuchemsha na
viazi vya kuchemsha"manumbu"na mihogo"mbute"

Tunawafundisha kula watoto wetu wafupi ili mrefuke,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…