Siempre Hechos
JF-Expert Member
- Dec 9, 2016
- 1,231
- 1,538
Yani huku, kipimo cha kushiba ni kula mpaka tumbo liume. Unakula mpaka inakosekana nafasi ya kuweka hata maji.
Hahahahahaha, ni kweli aisee!
Yani huku, kipimo cha kushiba ni kula mpaka tumbo liume. Unakula mpaka inakosekana nafasi ya kuweka hata maji.
Coast zone.Morogoro ni pwani ?
Mh hao wa Iringa? Ebu usitake kuleta ligi isiyo na msingi hapa jamvini. [emoji57]Wabena ndio wanashikilia rekodi ya ukarimu Tanzania.
Emoji zako tu zinaonyesha umetoka tangaMnajifanya wajuaji kumbe mnaharibu
Wakuu habari zenu leo nitaongelea hawa watani zangu wasukuma japo mimi ni mkazi wa morogoro, juzi juzi tulikua kijijini kwao na rafikiangu kwakweli tulipokelewa vizuri familia nzima ilikua na furaha ni familia yenye watu wengi tulionekana kua wageni kweli kweli niliona jogoo wawili wakubwa wamefungwa kamba
Badae rafikiangu alinitembeza kwenye mashamba yao hadi kwenye mbuga za mipunga jioni saa1 tulirudi nyumbani nikiwa nauchovu nikapewa maji ya kuoga saa2:30 msosi ulikua tayari na nilikua na njaa kinoma tulikua tumekaa pembeni kidogo na mwenzangu tukiwa tunachezea simu kupoteza mda alikuja dada mmoja akatukaribisha tukale,
Wasukuma wanadestuli ya kula kwa pamoja wanaume peke yao na wanawake nawao pia upande wao, upande wetu wanaume zilikuja sahani mbili za ugali kubwa na bakuli zilizo jaa nyama na maziwa mgando kwa pembeni, tukala navile mimi navoyapenda maziwa mgando nilikula sana, sasa mimi hapo mawazo yangu yalinituma nimalizie nyama niliokua nmeshikilia mkononi nitoshe
chakushangaza walikuja wadada watatu kutoka kule kwenye upande wa wanawake wakachukua vyombo vyote[emoji38][emoji38][emoji38] badae walikuja kiupya na sinia zilizo jaa nundu za ubwabwa(ubweche) na mabakuli makubwa yaliyojaa nyama za kutosha na soda moja moja kila mtu dah nilibaki naangalia tu maana mwanzo nlikua nmefukia vyakutosha rafikiangu akaniambia mbona umepoa tuendelee[emoji38][emoji38] niliutamani ubweche niligusagusa rakini sikua na namna, noma sana
Wasukuma nawapongeza mnamapokezi mazuri kwa wageni ila kwenye chakula hua mnaharibu maana najua chakula kilichobaki ni kingi mno isitoshe na asubuhi tulipikiwa chakula kingine nundu za ubweche.
=Exalioth
Tangu lini mkuu ?Coast zone.