Watani zangu wasukuma hebu punguzeni matumizi ya vyakula, mnaharibu

Watani zangu wasukuma hebu punguzeni matumizi ya vyakula, mnaharibu

Mimi nkikutana na msosi heavy kama huo nawaza vyombo hapo nimgetoa mshiko wafate wazunki au komoni
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]ulewe tena
 
Mnajifanya wajuaji kumbe mnaharibu

Wakuu habari zenu leo nitaongelea hawa watani zangu wasukuma japo mimi ni mkazi wa morogoro, juzi juzi tulikua kijijini kwao na rafikiangu kwakweli tulipokelewa vizuri familia nzima ilikua na furaha ni familia yenye watu wengi tulionekana kua wageni kweli kweli niliona jogoo wawili wakubwa wamefungwa kamba

Badae rafikiangu alinitembeza kwenye mashamba yao hadi kwenye mbuga za mipunga jioni saa1 tulirudi nyumbani nikiwa nauchovu nikapewa maji ya kuoga saa2:30 msosi ulikua tayari na nilikua na njaa kinoma tulikua tumekaa pembeni kidogo na mwenzangu tukiwa tunachezea simu kupoteza mda alikuja dada mmoja akatukaribisha tukale,

Wasukuma wanadestuli ya kula kwa pamoja wanaume peke yao na wanawake nawao pia upande wao, upande wetu wanaume zilikuja sahani mbili za ugali kubwa na bakuli zilizo jaa nyama na maziwa mgando kwa pembeni, tukala navile mimi navoyapenda maziwa mgando nilikula sana, sasa mimi hapo mawazo yangu yalinituma nimalizie nyama niliokua nmeshikilia mkononi nitoshe

chakushangaza walikuja wadada watatu kutoka kule kwenye upande wa wanawake wakachukua vyombo vyote[emoji38][emoji38][emoji38] badae walikuja kiupya na sinia zilizo jaa nundu za ubwabwa(ubweche) na mabakuli makubwa yaliyojaa nyama za kutosha na soda moja moja kila mtu dah nilibaki naangalia tu maana mwanzo nlikua nmefukia vyakutosha rafikiangu akaniambia mbona umepoa tuendelee[emoji38][emoji38] niliutamani ubweche niligusagusa rakini sikua na namna, noma sana

Wasukuma nawapongeza mnamapokezi mazuri kwa wageni ila kwenye chakula hua mnaharibu maana najua chakula kilichobaki ni kingi mno isitoshe na asubuhi tulipikiwa chakula kingine nundu za ubweche.

=Exalioth
Ndio jadi yetu hiyo, tena nyama ni chuku chuku
 
Hakuna watu wanakula sana kama wasukuma hakuna mfano Tanzania hii,Kabila Kama Wasukuma kwa kula.
Umekosea Hamna kabila wakarimu kama Wasukuma na Wanyamwezi Nchi hii ndio maana wakienda sehemu nyingine hubaki kushangaa tu!
 
Dah bc wasukuma mmetisha sanaa,, hii ya raund 2 mixa ugali na wali sio mchezo asee,
 
Karibu mkuu... Ndo maana sisi hatuoei mwanamke asopenda kulaa..tunaamini atakua ni mchoyo wa chakula.


Kuna jamaa, Na familia yake. Tuliwapelekaga kwa Babu zetu, hawakuamin pale walipochinjiwa Ng'ombe..mbuzi na kuku kuku, maziwa kama yote.

Ile asubuh tu mida ya saa nne..wameshiba mpaka wamechapa mboji[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ha ha mihayo ya wiza.
 
Hili spika ameliongelea,watanzania tuliowengi tu wavivu wakula ndiyo maana hata afya zetu za migogoro
 
Back
Top Bottom