bahati93
JF-Expert Member
- Aug 6, 2015
- 1,334
- 2,463
WATANIKUMBUKA SANA
Hivi nipo njiani narudi zangu jijini Dar es Salaam natoka mjini Mwanza ambako nimekaa kwa kipindi cha mwezi mzima Hotelini. Mwanza nilikuwa kikazi na katika kipindi chote hicho niliunda mazoea kwa Joana na Joel. Hawa ndugu zangu wawili nilikuwa nakutana nao kila nilipokuwa Napata msosi wangu pale lounge ya Hotel, walikuwa wanapenda kuja kila nilipochukua menyu.
Siku za kwanza wakati Napata chakula changu nilikuwa nawakaushia, nao wakawa wanazidi kunitolea macho na kunitazama navyokula kwa Uchoyo. Joel alikuwa hawezi vumilia kabisa, ni mara kwa mara nilishtukia amenigonga ukoko au amepiga kiti changu, ila joana yeye alikuwa ananikazia macho kichizi. Lakini hizo harakati zao zote zilikwama pale tu muhudumu alipokuwa akipita kwani wote walitimua mbio. Nilikuwa sijajua kwa nini hawa rafiki zangu wanawaogopa sana wahudumu wa pale mahala, nikaja kupata jibu mchana mmoja ambako muhudumu aliyekuwa zamu siku ile alimpiga na chupa Joel ambaye alikuwa pembeni ya jamaa mmoja mwenye kitambi akila chakula chake cha mchana.
Urafiki wetu ulianza siku ya saba nikiwa pale, nakumbuka siku hiyo nilikuwa na furaha sana hii ni baada ya kufanikiwa kuandika algorithm code ambayo ndio core ishue ya kazi iliyonipeleka Mwanza. Siku hiyo niliwapa sehemu kubwa sana ya samaki; Sato ambaye nilikuwa namla pamoja na ugali. Na jinsi navyowapa sio mkononi nawadondoshea tu chini, kulia au kushoto mwangu. Tangia siku hiyo nikawa nahakikisha nawapatia kile nachokula, ingawa wahudumu walikuwa hawapendi urafiki wetu, bali sisi tulikuwa tumeivana. Na katika kipindi hicho nilianza kujifunza tabia za hawa jamaa.
Nilingamua kwamba Jaona ni mtaratibu, yupo relaxed, muda mwingi unamkuta yupo smart na katika pose, hata nikiwa nakula msosi anakaa tu pembeni yupo assured kwamba nitampatia kidogo kitu hii ilipelekea kufikiria ya kwamba alizaliwa kipindi ambacho kulikuwa hamna njaa, au mamaye alimnyonyesha vyema ndipo alipojifunza uhimilivu wake. Lakini kwa Joel habari ni tofati yeye ni hatulii, ana wasiwasi sana nadhani amelizaliwa kipindi kuna njaa au mzazi wake hakuweza kumpatia maziwa vyema kama Joana ndio maana ana fujo sana. Mfano siku moja nimerudi jioni nina njaa nakula mara kanipiga kwenye paja! Kwa hasira na sauti nikamwambia “BRO SI USUBIRI MBONA HIVYO” hii ilipelekea wateja wengine pale kuniangalia kwa mashaka kidogo, but I don’t care sikupenda kwa kweli tabia mbovu ya Joel kwanini hatulii kama mwenzake. Yaani ana fujo sana sijui mnanielewa maana kuna siku nyingine tena mi nimemaliza kula samaki nanawa mara huyo akarukia juu ya meza na kutaka kuondoka na kichwa kizima cha Sato akaaishia kuchafua meza tuu, pumbavu sana.
Hata hivyo urafiki wetu haukuwa smooth kipindi chote hicho kwani kuna siku wamewahi nisaliti. Nakumbuka kama Kumbukumbu zangu zikiwa sawa siku tano kabda ya kuhitimisha kukaa kwangu alikuja jamaa mmoja yeye siku iyo alikuwa anakula Sato afu mimi nilikuwa nakula wali maharage na matunda, sasa nikashangaa hawana mpango na mimi kabisa wakawa wanajipitisha kwa jule jamaa, niliumia sana yaani siku zote nipo nao afu wananiacha kwa ajili ya samaki tuu.
Sasa ndo ivyo sijui kama ata wanajua kuwa nimeondoka maana nilikuwa sina namna ya kuwapa taarifa kwamba mimi ndo bye bye. Watanikumbuka sana kwa upendo mkumbwa niliowaonyesha, viumbe wazuri, wasafi, sharp na sifa kedekede.
Hizi apa picture zao you can tell a lot about them. Huyu chini ya kiti ni Joel na yule mwingine kwa pozi ni Joana.