Ni situ 365 yaani Mwaka mzima Tangu Meli ndogo ya mizigo MV AL.HUSSEIN II inayomilikiwa na bwana MAULANA SALUM ilipewa kibali Tarehe 3/4/2020 ikiwa na Watanzania 12 kutoka Zanzibar kupeleka sheena ya Mchele Msumbiji, haijarejea Zanzibar Tangu wakati huo pamoja na kwamba taarifa za kuufikisha mzigo huo zilipatikana
Jitihada za mmiliki wa Meli hiyo kupata usaidizi kwa Serikali ya SMZ watanzania wajulikane walipo na kurejea Zanzibar zimegonga mwamba na sasa anaiangukia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassani kuingilia kati ili Watanzania 11 ambao inasadikika wanashikiliwa na mamlaka za Msumbiji kurejeshwa Nyumbani.
Utata umeibuka baada ya Mfanyabiashara wa Mchele huo Bwana SAID SALIM ALEY (SAID DIGALAH) Kurejea Zanzibar wiki iliyopita bila wenziwe 11.