johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani umesema Serikali ina taarifa rasmi ya watu 24 wanaoaminika kuwa Watanzania wanaoshikiliwa na Mamlaka ya Uhamiaji na Forodha ya Marekani (ICE) kwa kuishi nchini humo kinyume cha sheria.
“ICE imetuarifu kwamba, watu wanne kati ya hao wameshakamilisha taratibu zote za kimahakama za kuondoshwa nchini Marekani, hivyo watarejeshwa Tanzania muda wowote kuanzia sasa. Watu 20 waliobaki wapo kwenye hatua mbalimbali za kesi zao za uhamiaji huko Marekani,” umeeleza ubalozi huo.
Ubalozi huo umesema hayo katika majibu ya maswali yaliyoulizwa na Mwananchi hivi karibuni kuhusu Watanzania waishio Marekani kinyume cha sheria.
Pia soma Hadi kufikia Novemba 24, 2024, Idadi ya watu waliopaswa kuondoka Marekani ni 1,445,549, wamo watanzania 301
Mwananchi