Watanzania 30,000 hufa kila mwaka kwa Hepatitis B".

Pinokyo Jujuman

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
552
Reaction score
104
Ugonjwa wa "INI" maarufu kama Hepatitis B ni ugonjwa hatari sana ambao huua takribani watanzania 30,000 kila mwaka; ugonjwa huu hauna tofauti sana na UKIMWI kwa jinsi unavyoambukizwa.
DALILI ZAKE: Mafua,Kuumwa kichwa,Homa,Kuchoka, na nyonde nyonde (Fatique),kukosa hamu ya kula chakula,kichefu chefu,Kutapika,maumivu kwenye tumbo na wakati mwingine unaweza kuharisha.

MAAMBUKIZI YAKE ni kama ilivyo HIV; natumai zama hizi hakuna asiyejua jinsi gani Virusi vya UKIMWI husambaaa.

Chukua Tahadhari Mapema"
 
Kwa hiyo huo ugonjwa tunaweza kuu-include kwa STD's??
 
Hii sasa ni balaaa, na wenyewe hautibiki au namna gani. Mimi nimeuguza wagonjwa wawili wa ini na kwa bahati mbaya wote walifariki, lakini wote walikuwa ni HIV case. Sasa ni vema ikawekwa wazi kama huo ugonjwa wa ini ni independent au ni makandokando ya HIV?
 

Ni kweli mkuu huu ugonjwa upo ila ni watu wachache sana wana taarifa zake,hata mimi nina mwezi wa pili tokea nipate taarifa za kuwepo kwa huo ugonjwa,ingawa nilipozama kwenye internet kuna maelezo ya baadhi ya madaktari wanao dai kuwa una dawa wakati wengine wakidai kuwa hauna dawa za kuponya zaidi ya kutuliza tu,jamani wana jamii wenzangu tuwe makini.
 
Ugonjwa huu sio kiambatanishi cha HIV ila ni ugonjwa independent unaweza kugoogle hepatitis B ukapata details au waweza tembelea hapa Hepatitis B Transmission, Symptoms, Causes, Diagnosis, Treatment, and Prevention Information by eMedicineHealth.com

Mimi niliuguza kaka yangu kabisa na bahati mbaya akafariki. Huu ni ugonjwa hatari sana na mara nyingi unagundulika very late na mbaya zaidi by the time unagundulika window period hadi ini linakufa kabisa kuwa ni 3-6 months (many of the acute cases zinaishia kwenye kifo) .

Kama tungekuwa na desturi ya kufanya checkup ingesaidia.
Uzuri nchi za nje kuna chanjo na nilibahatika kutembelea nchi fulani ulaya nikapatiwa chanjo.
Nawasihi wanajamii wenzangu wafanye uchunguzi zaidi ya ugonjwa huu maana by the time unaujua unao u are almost gone, bora hata HIV ukigundua unaweza ishi hata 20+ years.
 
Kwanini hapa kwetu hawaleti chanjo kama ipo? na kwanini kama tunapata misaada ya malaria isiwe pia ya ini? naomba jibu mkuu
 
Kwanini hapa kwetu hawaleti chanjo kama ipo? na kwanini kama tunapata misaada ya malaria isiwe pia ya ini? naomba jibu mkuu

Chanjo ipo. Mara nyingi akina mama wajawazito na watoto wachanga hupatiwa, pia madaktari na wauguzi hupata. Hata wewe ukitaka unaenda kwenye mahospitali ingawa itabidi ulipie. Muhimu ni kwamba wizara ya afya ingeaandaa programu ikatoa chanjo ya huu ugonjwa bure.
 
Duh mbona hatari zaidi ya HIV???? Ee Mwenyezi Mungu utunusuru!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…