Watanzania 7 kupeperusha Bendera ya Tanzania katika Olimpiki 2024 huko Paris

All the best, ila hapo pa kutoboa at least ni kwenye Riadha tukipambana sana...huko kwingine hatuna experience na mazoezi ya kutosha.
 
Tanzania sijui tunakosea wapi, sijui kwanini hatuoni michezo ni ajira pia tena ya maana. Kweli nchi ya watu Million zaidi ya 60 tunashindwa kujenga kikosi hata cha wachezaji 100, kujenga miundombinu kuwa serious na michezo mashuleni tujenge kizazi cha kiushindani mentality yetu iwe ya kushindana. Vijana wakiona wenzao wamefanikiwa watataka kuiga kama wanavyoiga kuimba. Ningekuwa mimi serikali ningeweka program za kufa mtu ili miaka 10 ijayo tuone matunda na kuendeleza system. Usikute tumewakilshwa wachezaji 7 ila viongozi 20.
 
Hatujui kama tutakuja kuwapata akina Filbert Bay,Seleman Nyambui,nk wa enzi za Mwalimu walioliletea Taifa heshima duniani.
Baada ya miaka hiyo tunapeleka Watalii.
Zimbabwe wamepelekwa wanamichezo 7 na Wasindikizaji zaidi ya 60! Sijui sisi ni wasindikizaji wangapi waliondamana na watu wetu!
 
Sikuhizi kuna Machawa wa Wanasiasa tu na Uzalendo wa kulazimisha
 
Utasikia timu itaambatana na maofisa 39.
 
Jana nilikuwa naangalia ufunguzi kuanzia SAA 1 usiku Hadi SAA 6 usiku hakika wenzetu wanajua Sana kuandaa ceremony zao..
Jinsi lile eneo lote la NORTE DAME CATHEDRAL na EIFFEL TOWER walivyodesign Kwaajili ya ufunguzi ilikuwa tamu Sana, timu zote shiriki zilikuwepo huku wakipita kwenye boti maalumu Kwaajili ya utambulisho

Tanzania tumepeleka timu ya watu wachache Sana wasiozidi watu 8 yaani wametuzidi Hadi Zimbabwe, Burundi na Malawi.
Wenye DStv ni muda wa kuenjoy huu umefika maana zile channels zote za super sport zimeshushwa kwenye package zote hadi kifurushi cha family
 
Wakristo duniani kote wamechukizwa na opening ceremony jinsi walivyodhihaki tukio la BWANA YESU AKILA LAST SUPPER NA WANAFUNZI WAKE( kwa wakatoliki hii ni sacrament takatifu).
Ufunguzi huu umeshirikisha mashoga wengi Sana kuanzia waimbaji, dancers na wale Queens.

Artistic director wa ceremony ni THOMAS JOLLY huyu SHOGA aliyekubuhu ni bilioena lkn ndiyo hivyo SHOGA, ingawa ufunguzi umetia fora duniani kote Kwa ubunifu wao Ila kasoro za kudhihaki Imani za watu zimetia doa
...hii ni baadhi ya picha zinalalamikiwa duniani
 
Nchi ina wananchi zaidi ya milioni 60+!!! Halafu katika mashindano yenye wanamichezo 10,000! Inapeleka wanamichezo 7 pekee!! Hivi nchi yetu ina kipi cha kujivunia?

Mheshimiwa Gerson Msigwa, wewe umekuwa Katibu Mkuu kwenye Wizara ya Michezo, Vijana na Utamaduni! Jambo hili unaona liko sawa kweli!! Miaka nenda Katibu Mkuu wa TOC ni Filbert Bayi!! Hivi hakuna watu wengine wenye mawazo mapya, wa kuongoza hiyo kamati ili tuone mabadiliko?
 
Nimeshangaa kuna michezo mpaka ya kulenga shabaa kweli hatuna wawakilishi?,kuogelea ndio mchezo unaniuma maana nilishawahi kukaa kisiwa cha ukerewe kama miezi miwili kuna miamba inaogelea kwa style mbalimbali ambazo hata olympic sijawahi kuona watu kama hao tusingekosa medal , mchezo wa kutupa mkuki nimesikia sina uhakika kuna kabila hapo manyara mambo ya mkuki na mishale wanajua kuliko kusoma na kuandika kama ni kweli kwanini wasitafutwe wakawa trained ?
 
Waogeleaji na wanariadha wanaowakilisha kila mashindano ni hao hao unategemea nini kipya kitatokea ? Hao ni watalii waliovaa jezi .
Kinachodidimiza michezo ni kuwa na viongozi wabovu wanaoangalia maslahi Yao na matumbo Yao tu .
 
Waogeleaji na wanariadha wanaowakilisha kila mashindano ni hao hao unategemea nini kipya kitatokea ? Hao ni watalii waliovaa jezi .
Kinachodidimiza michezo ni kuwa na viongozi wabovu wanaoangalia maslahi Yao na matumbo Yao tu .
Bila kusahau undugunization a.k.a nepotism na mambo ya uchama kwa kwenda mbele.
 
Tusubiri kusikia wanamichezo wa nchi maskini watakavyozamia huko ufaransa baada ya michezo.
Yaani kuna wanamichezo hawaendi kushiriki tu bali wana mipango yao ya kuzamia huko
 
Jana nimeona dada mmoja akipeperusha bendera ya ujerumani kwenye mbio za mita 1500 anaitwa MALAIKA MIHAMBO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…