Watanzania eleweni, CCM ni sikio la kufa. Dawa pekee ya kuwanyoosha kweli ni ICC tu

Watanzania eleweni, CCM ni sikio la kufa. Dawa pekee ya kuwanyoosha kweli ni ICC tu

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,491
Reaction score
57,973
Yaliyotokea Mbeya leo hivi ndivyo CCM ilivyo.

Anayoendelea kuyafanya Kenan kihongosi hivi ndivyo CCM ilivyo.

CCM haijutii vifo vya maelfu ya Watanzania kwenye Uchaguzi wa mwaka jana Oktoba 2025. Yaliyotokea waliyapanga na waliyaandaa maana ile ndo njia waliyopanga kuitumia ili wabakie madarakani.

CCM haijutii kutekwa na kupotezwa kwa mamia ya vijana wa Kitanzania wanaoikosoa Serikali yao, haijutii kufunguliwa kwa kesi za uongo wapinzani wao maana yote hayo yanafanyika kwa maelekezo yao na baraka zao.

CCM haijutii kuteswa kwa vyama vya upinzani, haijutii kuvunja Katiba ambayo inatambua nchi hii ni ya kidemokrasia haijutii na wala haiumii na jambo lolote baya linalofanywa kwa mtu ambaye hayupo upande wao.

Dawa pekee itakayowafundisha adabu CCM na Serikali yao ni kuhakikisha kwa namna zote, mauaji yaliyofanyika mwaka jana yanashughulikiwa Kimataifa hasa katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC na Mahakama nyinginezo za Nje.

Ni ICC tu itakayowafundisha CCM kuwa ukatili una malipo yake.

Ni ICC tu itakayowafundisha CCM kuwa mwananchi anapaswa kusikilizwa na kuheshimiwa matakwa yake.

Ni ICC tu itakayowafanya wanaotumwa na CCM kufanya ukatili dhidi ya Wananchi kuogopa kufanya ukatili dhidi ya Wananchi maana wataelewa matendo yeyote mabaya dhidi ya Wananchi yanaweza kusababisha wakaishia jela.

Ni ICC tu itakayowafanya CCM kurudi kutambua kuwa kumbe kuna haki za msingi za kikatiba za Wananchi wote na zinapaswa kuheshimiwa na kulindwa kweli.

Wito wangu kwa mara nyingine kwa Watanzania. Achaneni na CCM, nguvu zetu tuendelee kuziweka ICC. Tuwaunge mkono wanaotupigania kwenye ile Mahakama maana pale ndipo suluhisho lipo.

Mateso yote wanayotupitisha CCM kwa kutunyima haki zetu na kutuendesha kama watumwa kwenye Taifa letu yatakoma pale tu jambo la ICC litafanikiwa na CCM wakiona mwenyekiti wao, makada wao, watumishi wao wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa mara ya kwanza wanatolewa hati za kukamatwa na kufikishwa Mahakamani kwa mauaji waliyofanya dhidi ya Watanzania.

Tukio la leo Polisi kushusha benders za Chadema na kusikitisha Mkutano wao ilihali Kenani Kihongozi anatamba kama mwenye nchi kule Singida litufundishe kuwa dawa ya moto ni moto.
 
Back
Top Bottom