Watanzania hatujui kuweka kumbukumbu za kihistoria kwa faida

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
3,402
Reaction score
4,532
Juzi kuna kitongoji kidogo cha wingereza nilifungua mtandao nikaamua nikisome nione kuna nini .Kinaitwa Woolsthorpe Manor katika mji wa Grantham wilaya ya Lincolineshire.
Nikaona waliandika ndipo alikozaliwa mgunduzi mahiri aliyegundua mambo muhimu sana kwenye dunia ya leo ya mwendo na nguvu ya uvutano Sir ISAAC NEWTON.Pia ndipo alipozaliwa aliyekuwa waziri mkuu mwanamke wa kwanza wa wingereza MARGARETH THATCHER.
Nikaona nyumba aliyokuwa anaishi huyo mgunduzi na mama yake pembeni kidogo kuna mti wa mtufaa au tuseme Apple.
Inasemekana nguvu ya uvutano aliigundua alipokuwa likizo ya miaka miwili nyumbani kwao maana chuo kikuu alichokuwa anasoma cha Cambridge kilifungwa kutokana na kuibuka kwa ugonjwa wa Tauni.Siku moja alikuwa amekaa nje kwenye bustani yao akaona tunda linadondoka akajiuliza maswali mengi ni kwanini linadondoka kwenda chini? sio juu na kwanini limeshuka wima wima.Kuanzia hapo akaanza kufanya tafiti zake ndio akagundua kuna nguvu ya uvutano au gravity inavuta vitu vyote kwenda chini.
OK hizo ni story tu idea yangu ni kwamba huo mti wa mtufaa upo hadi leo na nyumba aliyoishi ipo hadi leo serikali ya wingereza iliamua kuutunza mti huo ulioibadilisha dunia na nyumba aliyokuwa anaishi iwe ni hazina na kumbukumbu kitaifa.Pengine utajiuliza miaka yote hiyo mti utaishije jibu ni kwamba walikuwa wanafany kitu kinaitwa marcotting yaani mti huo huo kizazi hadi kizazi wanakata tawi wanaweka mbolea wanapandikiza kuendeleza kizazi chake au wanachukua mbegu za mti huo kuzipanda tena eneo hilo hilo.
Kwenda kitongoji hicho kuna gate limejengwa na ndani kuna cafe,bar na viburudisho mbali mbali ili kwenda eneo hilo unalipia gharama kama mtalii serikali inapata mapato.
Sasa tuje nchini kwetu kuna makaburi ya watu mashuhuri mfano Shaban Robert,Mkwawa fuvu lake na wengine wengi je ili kuwaenzi na kupata kipato hatuwezi kufanya makaburi yao au basi kama kuna dini zinakataza hata nyumba walizokuwa wanaishi zikafanywa sehemu ya makumbusho?.
Mwanza kuna mahali niliona mwenge na nyumba mbovu mbovu karibu na ziwa Mkuyuni kibao kilichoandikwa mahali alipolala mwalimu Nyerere alipokuwa anatafuta Uhuru.Msukuma mmoja alijitolea kumfadhili kulala usiku huo maana angeenda mjini wazungu wangemkamata.Huo ni mfano mzuri

Kile kimondo cha Mbozi nacho kingefanyiwa mpango huo kijengewe vizuri kwenda pale unalipa ushuru.Wazungu wana msemo wa kutudharau waafrica kuwa ukitaka kumficha muafrica kitu usipate shida wewe ficha kwenye kitabu kwa maandishi hatasoma.
Picha chini ni mti huo na nyumba ya ISAAC NEWTON alizaliwa mwaka 1643 na kufariki 1727
Hatujachelewa tutafakari
 
Attachments

  • woolsthorpe manor.JPG
    woolsthorpe manor.JPG
    82.2 KB · Views: 5
Mti ni kiumbe hai kinaishi, we unataka watanzania waenzi makabuli ya wafu😂.
Mbona wewe babu yako au baba yako aliyekufa mkimzika mnaweka alama tu na wakati mwingine mnaandika hadi jina alizaliwa lini na kufa lini.
It is just a matter of memory.Je ukiambiwa baba yako,ndugu yako au babu yako amekufa wewe uko mbali unaweza waambia mtupeni tu porini aliwe na fisi? na ajabu mtaingia gharama kumsafirisha wakati ni mfu hana tofauti na jiwe tu bora mti una uhai.
Ni mila tu bro najua imani za dini tunatofautiana.
Hivi unafikiri kwanini wachaga mwezi wa 12 wanapenda kwenda kwao.Sababu kubwa ni kwenda kuenzi kwao ikiwemo kutembelea makaburi ya wafu wao hii inaleta unification na mshikamano kwa taarifa yako hata wazungu wako hvi.Jiulize kwanini Dr David Livingstone alifia Zambia na bado akaenda kuzikiwa kwao wingereza?
Ukiona kabila flani hawajali sana makwao na kuenzi wafu wao hata maendeleo yao ni muflisi kabisa
 
Juzi kuna kitongoji kidogo cha wingereza nilifungua mtandao nikaamua nikisome nione kuna nini .Kinaitwa Woolsthorpe Manor katika mji wa Grantham wilaya ya Lincolineshire.
Nikaona waliandika ndipo alikozaliwa mgunduzi mahiri aliyegundua mambo muhimu sana kwenye dunia ya leo ya mwendo na nguvu ya uvutano Sir ISAAC NEWTON.Pia ndipo alipozaliwa aliyekuwa waziri mkuu mwanamke wa kwanza wa wingereza MARGARETH THATCHER.
Nikaona nyumba aliyokuwa anaishi huyo mgunduzi na mama yake pembeni kidogo kuna mti wa mtufaa au tuseme Apple.
Inasemekana nguvu ya uvutano aliigundua alipokuwa likizo ya miaka miwili nyumbani kwao maana chuo kikuu alichokuwa anasoma cha Cambridge kilifungwa kutokana na kuibuka kwa ugonjwa wa Tauni.Siku moja alikuwa amekaa nje kwenye bustani yao akaona tunda linadondoka akajiuliza maswali mengi ni kwanini linadondoka kwenda chini? sio juu na kwanini limeshuka wima wima.Kuanzia hapo akaanza kufanya tafiti zake ndio akagundua kuna nguvu ya uvutano au gravity inavuta vitu vyote kwenda chini.
OK hizo ni story tu idea yangu ni kwamba huo mti wa mtufaa upo hadi leo na nyumba aliyoishi ipo hadi leo serikali ya wingereza iliamua kuutunza mti huo ulioibadilisha dunia na nyumba aliyokuwa anaishi iwe ni hazina na kumbukumbu kitaifa.Pengine utajiuliza miaka yote hiyo mti utaishije jibu ni kwamba walikuwa wanafany kitu kinaitwa marcotting yaani mti huo huo kizazi hadi kizazi wanakata tawi wanaweka mbolea wanapandikiza kuendeleza kizazi chake au wanachukua mbegu za mti huo kuzipanda tena eneo hilo hilo.
Kwenda kitongoji hicho kuna gate limejengwa na ndani kuna cafe,bar na viburudisho mbali mbali ili kwenda eneo hilo unalipia gharama kama mtalii serikali inapata mapato.
Sasa tuje nchini kwetu kuna makaburi ya watu mashuhuri mfano Shaban Robert,Mkwawa fuvu lake na wengine wengi je ili kuwaenzi na kupata kipato hatuwezi kufanya makaburi yao au basi kama kuna dini zinakataza hata nyumba walizokuwa wanaishi zikafanywa sehemu ya makumbusho?.
Mwanza kuna mahali niliona mwenge na nyumba mbovu mbovu karibu na ziwa Mkuyuni kibao kilichoandikwa mahali alipolala mwalimu Nyerere alipokuwa anatafuta Uhuru.Msukuma mmoja alijitolea kumfadhili kulala usiku huo maana angeenda mjini wazungu wangemkamata.Huo ni mfano mzuri

Kile kimondo cha Mbozi nacho kingefanyiwa mpango huo kijengewe vizuri kwenda pale unalipa ushuru.Wazungu wana msemo wa kutudharau waafrica kuwa ukitaka kumficha muafrica kitu usipate shida wewe ficha kwenye kitabu kwa maandishi hatasoma.
Picha chini ni mti huo na nyumba ya ISAAC NEWTON alizaliwa mwaka 1643 na kufariki 1727
Hatujachelewa tutafakari
𝐔𝐤𝐨 𝐬𝐚𝐡𝐢𝐡𝐢 𝐤𝐚𝐛𝐢𝐬𝐚

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mti ni kiumbe hai kinaishi, we unataka watanzania waenzi makabuli ya wafu😂.
Usichanganye dini hasa ukristo na mambo ya kisasa acha hizo mbona pango alilozikwa YESU na kaburi la mtume Muhamad liko hadi leo hizi dini zilizoingiliwa na freemason zinatupa tabu sana na ndio maana siku hizi watu wanajiita manabii
 
Back
Top Bottom