Watanzania hatujui wajibu wa Viongozi wetu, au tumeweka vigezo vya chini kuwapima

Watanzania hatujui wajibu wa Viongozi wetu, au tumeweka vigezo vya chini kuwapima

MAKULUGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2011
Posts
7,828
Reaction score
10,527
Mada hii aliwahi kuandika... Prof.Mkumbo (kabla hajakengeuka!) kuwa tumeweka viwango vya chini mno kuwapima viongozi wetu!

Ukifuatilia mijadala inayoendelea hapa nchi kuhusu masuala nyeti kama umeme, maji, kilimo, nk utabaini jambo hili!

Mfano mdogo tu, ni lawama zinazoelekezwa kwa Januari Makamba kuhusu tozo, bei ya Mafuta, TANESCO ni kama vile amekuwa Waziri Kwa miaka 10!

Hivi ni kweli tatizo ni Makamba au kuna shida ya uongozi kwenye eneo hilo?

Nini Sera ya Serikali ambayo Makamba tunampima nayo tujue kama anauweza au la! Mbona hatujiulizi CCM kama Chama Tawala kina Sera gani na maono gani ya kutupeleka mbele!

Kwanini tunakimbilia kuwashambulia watu binafsi badala ya Mfumo!

Kwa hali ilivyo, tusishangae kila mwaka Tukitawaliwa na kundi dogo la watu ambao wanajua Watanzania Hatujui tunataka Nini, Wala tutakipataje!

Sina ushabiki na Mwana CCM YOYOTE KWA SABABU NAJUA AWE SUKUMA GANG,CHATO ,MSOGA AU ......NDIO CHANZO CHA MATATIZO YOTE HAYA AMBAYO TUNAJADILI.KWA.UPEO.MDOGO MNO!
 
Back
Top Bottom