Kinachomfelisha ni uzungu tu hakuna kingine, hakuna msanii aliyewahi kutoboa bongo kwa swaga za kizungu, lazima ajue anadeal na watu gani. Hata bwanaake Jux hawezi kutoboa bongo kwa aina ile ya mziki anayoifanya, na uhakika hata Shilole mziki umemnufaisha kuliko Vannesa, ni kwakuwa mziki wake unaendana na watanzania japo kipaji chake hamfikii hata robo Vannesa. Navy Kenzo na wenyewe walikuwa wazungu sana, ila tangu wametoa kamata chini wamefanikiwa kuturoga wabongo, sahvi wanapiga show kila wiki, abadilike kama anataka kufanikiwa kwny mziki, sio anatoa audio ya kiswazi ila video zimejaa uzungu, ataendelea kusubiri sana