Watanzania hatuna mtetezi. Kampuni za simu zinafanya zitakavyo

Watanzania hatuna mtetezi. Kampuni za simu zinafanya zitakavyo

Hili ni soko huria
Mkuu Africa kwenye makampuni ya simu hamna soko huria. Ni kama Cartel flanj hivi na bajonga kichiz hela ndefu makampuni yasiwe mengi na wote kwa pamoja wahafikiana kutoza bei.
 
Ni ngumu kupata mtetezi ktk hili japo linajulikana hadi kwa wakuu wote.
Anyway, The beautiful one' is not yet born
Nilidhani are not yet born?! Ni kama tu ile all that glitters is not gold mara ya kwanza nilidhani are not gold. Muingereza mpuuzi sana yani anatuchanganyaga kichiz
 
tatizo ni pale walipofikiri kila anae ingia kwenye internet basi anaenda kutazama ngono bila kujali kuna wanaoingia kusoma na kufanya biashara,
Hahahahhaa kwamba ndio sabb wamepandisha au utawala mbovu
 
Zamani nilikuwa naumia kama wewe.

Badae nikaona nisitoe huduma zote kwa kampuni 1 tu.

Internet nachukua Smile, Dakika nachukua Vodacom na sms nachukua Tigo.

Smile kidogo wapo stable kwenye huduma zao. Kwa mwaka wanaweza badilisha vufurushi mara 1 au 2. Na wanatoa offer kibao tu.
Naweza kuamini ila bado si dawa
 
Hilo kitira mkumbo hakuwaza wala kabudi
 
Sitaki kuamini kwamba, Kuna namna moja au nyingine ambayo huyu waziri wa sasa wa sekta hii ananufaika na hili au BIG GUNS wa mashirika hayo ni watu wake wa karibu na hana uwezo wa kuwafanya lolote.
Biashara hii sasa inaendeshwa kama magenge ya dawa za kulevya. Biashara ambazo unakuta wasemaji wote wa wananchi wapo kwenye payroll za magenge ya hayo na hakuna atakayeweza kuwatetea.

Si mara moja nimewahi kumsikia waziri huyu akitetea unyonyaji unaofanywa na makampuni haya kwa kulinganisha thamani ya fedha na nchi nyingine bila kujali kuwa uchumi wa nchi hautafsiriwi na fedha, bali fedha hiyo inaweza kununua nini.
USA wanaweza kununua GB 1 kwa shilingi 4,000 za kitanzania, lakini kwao kuipata USD 1.7 ni rahisi kuliko kutafuta pesa sawa na hiyo hapa kwetu, ambayo ni 4000 Tsh.

Kuna watu wanafanya kazi za viwandani wanalipwa Tsh 5000 kwa shifti, kuna wasaidizi wa migahawa wanalipwa Tsh 4,000 kwa siku.
Tatizo linakuja pale watu wanaokuja na mapendekezo ya gharama za huduma hizi, hawajui lolote kuhusu jinsi Watanzania wa hali ya chini wanavyoishi..

Katika kipindi hiki cha mabadiliko ya kidijitali, huduma ya mtandao kwa sasa ni moja ya mahitaji muhimu katika uchumi wa nchi yoyote ile, kama ilivyo kwa mafuta, ingawa watu hawaoni kuwa kuna njia ambayo ongezeko la gharama hizi litaanza. kuathiri bei za vitu vingine.
 
Dah nimeshangaa sana, maana mm ndiyo kifurushi changu nanunuaga hicho. Nimejaribu kununua jioni hii nakuta 2.7gb nikachoka nikawa sina namna ikabidi ninunue tu kishingo upande. Yaani wanabidilisha tu wanavyojisikia bila hata kutoa taarifa, hii mbaya sana. Kwa mwendo huu tutatoboa kweli, huku matozo kila mahali, huku mavifurushi
Bado hujashtuka kwann mkuu?
Wamegundua information znasambaa sana through data.. hata mapinduz ya srilanka yalichajiwa na mtandao.. so .. lawama zote za uchumi mbovu unaoporomoka na taarifa zmekua ndio hoja mtambuka kwasasa. So kimkakat wanajarib ku discourage hilo kwa kufanya watu wasiwe mtandaon muda mref yaan wasiwe na access ya taarifa muhimu
 
Kweli kabisa, nilikuwa nanunua bando la mwezi mzima 22GB kupitia Airtel kwa Tsh 30,000. Kwa hela hiyo hiyo wakaanza kupunguza bando hadi19.5GB. Hadi sahivi kwa hela hiyo hiyo wameweka 16.5GB [emoji38][emoji38][emoji38] Duh I see!!
 
Sasa wote tukiwa wanasiasa kada zingine nani atabaki?
Ndg "Maghayo" kwanza naambiwa maana ya avatar name yako ni "Dharau" okay twende kwa mada.

Nimemjibu yule aliyehoji that's why sikuandika "ushauri wangu kwenu" bali (kwako) mean niliye_reply kwake.

Karibu.
 
Dah nimeshangaa sana, maana mm ndiyo kifurushi changu nanunuaga hicho. Nimejaribu kununua jioni hii nakuta 2.7gb nikachoka nikawa sina namna ikabidi ninunue tu kishingo upande. Yaani wanabidilisha tu wanavyojisikia bila hata kutoa taarifa, hii mbaya sana. Kwa mwendo huu tutatoboa kweli, huku matozo kila mahali, huku mavifurushi
Ni kampuni zote tu balaaa
 
Niseme wazi hili jambo wabongo tumetelekezwa hatuna mtu wa kukemea unyama unaofanywa juu yetu.

Tigo wamebadilisha vifurushi kwa wiki elfu tano inakuwa gb 2.7 badala ya gb 3 na watu wanaotakiwa kututetea wamenyamaza kabisa.

Dah nawaza nakosa majibu

Na hayo ni maelekezo ya aliyepaswa kuwa mtetezi wa wananchi kwa mitandao ya simu lengo ni ifike GB 1 kwa 10k
 
Daah Tanzania kuhusu bando tunaibiwa sana sana hata hizo dakika za kupiga ukinunua unaambiwa dk kadhaa ila zinapotumika wanatoa kwa idadi ya sekunde ni ngumu kujua unachokitumia baada ya siku chache hata ukiweka simu mezani usiitumie utaambiwa zimeisha wakikukosa hapo unakutana na expire ya kifurushi muda mwingine hata kabla ya wiki au mwezi kufika ukiwapigia simu ndio kwanza nao wanakuuliza tena...
 
Ndg "Maghayo" kwanza naambiwa maana ya avatar name yako ni "Dharau" okay twende kwa mada.

Nimemjibu yule aliyehoji that's why sikuandika "ushauri wangu kwenu" bali (kwako) mean niliye_reply kwake.

Karibu.
Nimecheka balaa
 
Mnalalamika nini situlikubaliana kwamba ambaye anaona hatendewi haki ahamie Burundi? mnaboa sana nyinyi na ndio wale wale mliokua mnasema mama anaupiga mwingi
 
Mnalalamika nini situlikubaliana kwamba ambaye anaona hatendewi haki ahamie Burundi? mnaboa sana nyinyi na ndio wale wale mliokua mnasema mama anaupiga mwingi
Aliyesema hayo hakuna anacholipa kutoka kwenye hela ya mshahara wake na wala kodi wala bima wala nssf halipi na ana mikopo bila masharti
 
Back
Top Bottom