Watanzania hatuna mtetezi. Kampuni za simu zinafanya zitakavyo

Niseme wazi hili jambo wabongo tumetelekezwa hatuna mtu wa kukemea unyama unaofanywa juu yetu.

Tigo wamebadilisha vifurushi kwa wiki elfu tano inakuwa gb 2.7 badala ya gb 3 na watu wanaotakiwa kututetea wamenyamaza kabisa.

Dah nawaza nakosa majibu
Utetewe na Nani wakati waterezi ndio wenye hisa? Nchi ngumu hii
 
Them Say It Doesn't Matter What Your Feelings and Thinking Are !!!!!
 
Makamba analamba asali HALOTEL
Rostam analamba asali vodacom na wenzake

We unadhani nani atakutetea hapo wakati walamba asali wapo kazini.
 
Airtel nanunua bado la internet leo saa 4 asubuhi la wiki GB 1.2,sas 7 mchana nanunua bado la kupiga mitandao yote la wiki sh.1500 napewa Mb70. saa 12 jioni naambiwa kufurushi chako cha internet kimeisha.Nahitajika kununua bando la internet.Huu si wizi.Kwanini wasifungiwe.Kunasiku inakuja.
 
Kwa kweli yaani!

Halafu cha kushangaza waziri anasimama na makampuni anawaacha wananchi.
 
Kero mojawapo:

Unajiunga kifurushi ujumbe unakwambia salio halitoshi,

Lakini ujumbe hausemi kiasi cha salio lililopo ambalo halitoshi,

Inakutaka Eti utafute kujua salio ili wakukate vihela vyako [emoji848][emoji2356]
 
TCRA ndio shida, inawapangia bundle ndogo ili wazidi kukusanya Kodi kiharamia
 
Hivi wenye hisa hela huwa haziwatoshi tu.halotel wameshusha MB kwenye vifurushi,sasa hivi namimi napunguza matumizi tu! Hii balaa...
 
tatizo ni pale walipofikiri kila anae ingia kwenye internet basi anaenda kutazama ngono bila kujali kuna wanaoingia kusoma na kufanya biashara,
Sababu ni kuongezeka kwa Kodi kwenye vifurushi.
Hivyo makapuni yanaongeza bei ili yaweze kupata faida, hawawezi kukemewa Kwasababu wote wawili wanajua kinachoendelea. Ila sisi walaji ndio hatujui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…