Watanzania hawamchukii Magufuli, wanaichukia CCM kwa sababu ya rushwa kukithiri

Watanzania hawamchukii Magufuli, wanaichukia CCM kwa sababu ya rushwa kukithiri

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,255
Reaction score
8,027
Chama changu kinachukiwa na wananchi kutokana na kukithiri kwa vitendo vya rushwa kukithiri. Wananchi wanahisi kubadili chama huenda ndio suluhisho la maisha bora kwao.

Pamoja na ukali wa Mwenyekiti wetu wa chama taifa kuhusu Rushwa, lakini kwa sasa Rushwa ndio kwanza inazaliwa CCM.

Sisi wanaCCM asili tunauliza, kama Rais alipigiwa kelele miaka yote 5, lakini hii 2020 CCM ndani ya chaguzi kura za maoni rushwa ndio kwanza kama imezaliwa vile.

Haya yamesemwa jana na mzee JOSEPH BUTIKU Mwanaccm mwenzangu. Sasa kama tutapata wabunge wala Rushwa watamsaidiaje Rais wetu? Kama wote hawa wamepita kwa rushwa na kamati za CCM zikawarejesha, hiyo serikali itakuaje?

CCM tumeshindwa kuonesha kwa vitendo kuikataa rushwa tutaaminiwaje?
 
Kwa kweli ni aibu kubwa! Nimeamini yasemwayo. Ally Keissy Mohamed kupitishwa tena na Halmashauri kuu ya Taifa? Hakika usiamini asemacho mtu mweusi!
 
Kwa nini unawasemea WaTz wote kama vile kweli!
Si rushwa tu nyoosha maelezo Mkuu
WaTz wamejawa na woga hakuna uhuru wa chochote Mnawanyanyasa watu mnawatesa watu mnawapoteza watu

Watu wanaishi kama digidigi nchini mwao kwa sababu ya dhuluma ya utawala na chama chake

Rudia kuandika nyoooosha maelezo tusipakane mafuta kwa mgongo wa chupa
Kuna Wafalme na Watumwa katika Taifa
 
Tatizo aliyekuwa anapinga rushwa ni JPM peke yake. Hakujenga mfumo thabiti wa kupambana na rushwa ndani ya chama. Akabaki na mfumo wa mikwara ya Polepole na mzee wa kuoainisha kura ulizopata na matukio yaliyokupa kura. Rushwa ni mfumo, na ili upambane nayo unahitaji mfumo thabiti. Bahati nzuri CCM ina taasisi nyingi imara, mfano wangeweza kuwatumia green guard au UVCCM au VYUO NA VYUO VIKUU wakaunda command ya anticorruption na rushwa ingedhibitiwa ndani ya chama bila kutumia takukuru. MKT unda mfumo wa kudhibiti rushwa, vitisho bila mifumo ni kazi buree
 
Ilijitajika rushwa kiasi gani kufanya uchunguzi wa shambulizi la Tundu Lissu?
 
Mimi Ni mmoja wapo ninayemchukia huyu mzee na Nina sababu kumi za kumchukia huyu mtawala!

Kama Ni rushwa mbona nchi nyingi tu Kuna rushwa na zimetamalaki.
 
Kwa hiyo Magufuli kaanza kutawala kwenye kura za maoni za CCM? Wewe Kama umrpigwa chini kura za maoni usilete mihasira kwa Magufuli hapa.Keani yeye ndie aliyekuwa alipiga kura au kuwapa fomu za Kugombea watia Nia?

Umebwagwa Huko chini unamsikumia mihasira yako Magufuli sukumia wapiga kura Wala rushwa

Kama uliona rushwa kwa Nini hukuripoti Takukuru? Wewe Sio CCM
 
Tatizo siyo ccm. Ni aina ya wanaccm waliomo kwa sasa. Kwani Nyerere hakuwa ccm?
CCM ya Sasa inaongozwa na watu kama:-
Magufuli. Kweli?
Polepole. Are you serious?
Bashiru. Of all the people?
Halafu eti Ndugai, Tulia ndiyo wanaCCM wanao ongoza mhimili wa bunge. Jamani??!!
 
Back
Top Bottom