Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Licha ya kuwepo kwa mwamko wa wananchi kujenga nyumba kupitia fedha zao za mfukoni, hali inaonyesha kuwa huwachukua wastani wa miaka kumi hadi miaka 15 kumaliza kujenga nyumba hizo.
Hayo yameelezwa leo Ijumaa Agosti 9, 2024 na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Hamad Abdallah.
“Mpaka sasa asilimia 99 ya Watanzania wanajenga nyumba kupitia fedha za mfukoni mwao ambazo nyingi ni zile za kudunduliza na hivyo kuchukua muda mrefu kuzimaliza,’’ amesema.
Watanzania wengi wanaishi kwenye nyumba zinazoendelea kujengwa
Ni kutokana na hilo amesema wengi wao huishi katika nyumba ambazo bado hazijamalizika na pale wanapopata fedha, humalizia chumba kimoja kimoja wakiwa ndani.
Pia Abdallah amesema takwimu pia zinaonyesha mpaka sasa kuna uhaba wa nyumba milioni 3.8 huku uhitaji wa nyumba kila mwaka ukiwa ni 3000 na kati ya nyumba hizo zipo za kupanga au za kununua.
“Ukiangalia kwa kazi tunayoifanya tunatakiwa kupambana na uhitaji wa watu wa nyumba hizo lakini wakati huohuo kuangalia ongezeko la watu na kuitumia kama fursa katika biashara ya nyumba.
“Takwimu zinaonyesha kuwa hadi kufika mwaka 2050, asilimia 44 ya Watanzania watakuwa wanaishi mjini na hali hiyo imeanza kujionyesha namna Dar es Salaam kwa sasa ilivyojaa na wengi huishi mkoani Pwani na kuja kufanya kazi Dar es Salaam.
“Vilevile kuanza kwa mradi wa treni ya umeme tutegemee watu wengi wataishi Morogoro na kuja kazini Dar es Salaam,” amesema Abdallah.