Watanzania ilitokeaje mkaishia kubadilishiwa kibao na Barrick kwenye madini, hadi mkaangukia pua?

Watanzania ilitokeaje mkaishia kubadilishiwa kibao na Barrick kwenye madini, hadi mkaangukia pua?

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Licha ya makelele yote yale na mamia ya nyuzi humu JF na nenda rudi nyingi zile baina ya serikali yenu na Barrick, ilifikaje makubaliano ya 2017 kupinduliwa na kufanywa kinyume chake, niwe mkweli hayo makubaliano ya awali yalinifanya nihisi kwa namna fulani Magufuli ndiye kiboko na starring wa movie dhidi ya mabeberu, na ndiye atakua rais wa kwanza Afrika kusimamia kidete kile anakiamini kuwa maslahi ya Watanzania, ila hii video ya BBC inaonyesha mliangukia pua na mkarudi kwenye chini ya miguu ya mabeberu.

Inatia huruma, hili sio la kuchekwa maana huu ukata na umaskini Afrika umetamalaki licha ya utajiri wa raslimali.

walisaini hadharani,leta walau picha tu wakiubadilisha,wakenya tunajua mnajipenyeza mpaka BBC huko ili tu kutudhalilisha

Unatia huruma mataga hadi nimecheka ujue.
 
Magu kacheza kama Pele kwenye hili hasa kwenye wachimbaji wadogo ambao ndio mchango wao unaingia moja kwa moja kwa mwananchi wa kawaida, Geita sasa ni mji wa mamilionea, nimesikia moja ya makubaliano ya Ndaishimiye na Magufuli ni madini yote ya Burundi kuja kuuzwa Tanzania, Malawi pia walishalimaliza hilo

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Magu kwenye suala la madini hana mfanowe.

Geita tu inaingiza billion 14 kutoka billion 1 kabla.

Kuna mtu anaweza kutuambia kwamba serikali inapata kiasi gani kwenye madini kuhusu wale mabeberu?
 
Ngai fafa!! Hawa watu kumbe magufuli anajua kuwabeba makodofia! Ama ni kizungu ilimpita!
 
MK254,

..kwanza zilitoka ripoti zinazosema accacia wametuibia na tunawadai usd 191 billion.

..serikali na barrick wakafanya "mazungumzo", halafu wakaenda Ikulu kwa Raisi wakatangaza watatulipa usd 300 million.

..sasa ukiibiwa usd 191 billion halafu ukakubali kulipwa usd 300 m, mathematically, ni sawa na mtu aliyeibiwa usd 636 halafu akakubali kulipwa usd 1.
 
Mlitakeje kwani? yaendelee tu kupita bandarini na mkoa wetu ubakie mashimo.
 
MK254,

..kwanza zilitoka ripoti zinazosema accacia wametuibia na tunawadai usd 191 billion.

..serikali na barrick wakafanya "mazungumzo", halafu wakaenda Ikulu kwa Raisi wakatangaza watatulipa usd 300 million.

..sasa ukiibiwa usd 191 billion halafu ukakubali kulipwa usd 300 m, mathematically, ni sawa na mtu aliyeibiwa usd 636 halafu akakubali kulipwa usd 1.

191B ni ukijumuisha GDP ya mataifa ya Afrika Mashariki, dah. Halafu hata hiyo 300m naona haiji kama ilivyokubaliwa awali. Very sad.
Lakini unahisi suluhu ni nini, maana sio kwa mikwra yote aliyochimba Magufuli na jamaa hawakutetereka wala kuyumba au hata kubadilika chochote cha maana, je upinzani ndio watafanya nini tofauti.
 
191B ni ukijumuisha GDP ya mataifa ya Afrika Mashariki, dah. Halafu hata hiyo 300m naona haiji kama ilivyokubaliwa awali.....very sad.
Lakini unahisi suluhu ni nini, maana sio kwa mikwra yote aliyochimba Magufuli na jamaa hawakutetereka wala kuyumba au hata kubadilika chochote cha maana, je upinzani ndio watafanya nini tofauti.

..tulikosea kutengeneza ripoti ambazo sio za kweli.

..ripoti zingekuwa za kweli, na siyo rahisi kuwa disputed, tungeweza kupata haki yetu.
 
Back
Top Bottom