Tulipofikia Watanzania, wenzetu huita rock bottom wakiwa na maana kwamba tulipofika hatuwezi kwenda chini zaidi. Tumegota kwenye mwamba.
Fikiria unaagiza mtungi wa gesi na ghafla huo umetua mlangoni...
Unaagiza kreti ya soda mbalimbali na hiyo imetua mlangoni...
Unampa kazi fundi bomba na jioni ukirudi, kazi hiyo imeisha!...
Sasa shuhudia maajabu juu ya maajabu…
Unapata wageni nyumbani kwako wanapita karibu na mtungi wa gesi, hakuna anayeshtuka wala kuulizia vipi huo mtungi, mbona kama umeokotwa dampo?
Unasogeza kreti na kuwafungulia soda, hakuna anayejali uchafu unaoonekana wazi kwenye kreti hata kwa kipofu! Watabugia soda utadhani wana kiu ya kufa mtu.
Sasa tuje kwenye siasa na uongozi. Je nako tumefika rock bottom? Tunaona kabisa chama kimechoka, kichafu na hakina tena sifa wala uwezo wa kuendelea kuwa madarakani lakini twende tu. Tunakimwagia sifa.
Tunaona kabisa kwamba kiongozi fulani ni limbukeni hatufai lakini sawa tu. Au ni kweli wasemavyo wenzetu, mapenzi hupofusha?