Bado natafuta sifa sahihi ya kuwapa Watanzania wa leo lakini nashindwa. Hebu fikiria, mtu unaweka pesa zako benki ukitegemea utatengeneza faida kwa kuipa benki hiyo mtaji. Badala yake benki ndiyo inakukata hela kwa kutumia hela zako bila idhini yako.MAMBO NI MENGI SANA HII NCHI YA KINA OIERRE LIKWIDI
Hao wapuuzi na wajinga ndio mtaji wa CCM. Wezi wakiwa mezani wanakula vinono, hao wako chini ya meza wakitupiwa mifupa na kuvikwa vilemba vya ukoka.Hii nchi watu wapuuzi wapuuzi ndio wanaopata umaarufu wewe unategemea nini...shishi baby, pielle liquid, amber luth, posh queen
wanaofaidika na mfumo huo "mchafu" ndio wanamwaga sifa. Ukipinga as Chadema is doing unaishia kupigwa risasi/kufungwa/kupewa ugaidi/ kubambikiwa case in a compromised judicial system etc etc. sasa tunafanyaje, wote kuondokana na hili dubwasha?Tunakimwagia sifa.
Wachovu sana sisi fikiria sasa ivi kuna huyu mandonga anawatu wakutosha wanamfatiliaMAMBO NI MENGI SANA HII NCHI YA KINA OIERRE LIKWIDI
Tulipofikia Watanzania, wenzetu huita rock bottom wakiwa na maana kwamba tulipofika hatuwezi kwenda chini zaidi. Tumegota kwenye mwamba.
Fikiria unaagiza mtungi wa gesi na ghafla huo umetua mlangoni...
View attachment 2409951
Unaagiza kreti ya soda mbalimbali na hiyo imetua mlangoni...
View attachment 2409956
Unampa kazi fundi bomba na jioni ukirudi, kazi hiyo imeisha!...
View attachment 2409962 View attachment 2409963
Sasa shuhudia maajabu juu ya maajabu…
Unapata wageni nyumbani kwako wanapita karibu na mtungi wa gesi, hakuna anayeshtuka wala kuulizia vipi huo mtungi, mbona kama umeokotwa dampo?
Unasogeza kreti na kuwafungulia soda, hakuna anayejali uchafu unaoonekana wazi kwenye kreti hata kwa kipofu! Watabugia soda utadhani wana kiu ya kufa mtu.
Sasa tuje kwenye siasa na uongozi. Je nako tumefika rock bottom? Tunaona kabisa chama kimechoka, kichafu na hakina tena sifa wala uwezo wa kuendelea kuwa madarakani lakini twende tu. Tunakimwagia sifa.
Tunaona kabisa kwamba kiongozi fulani ni limbukeni hatufai lakini sawa tu. Au ni kweli wasemavyo wenzetu, mapenzi hupofusha?
Kizazi kijacho ambacho kitapita kwenye mfumo huu huu wa elimu au?Ukiona hayo yote uliyoorodhesha yanatokea na hakuna anayeuliza chochote, basi ujue hata uwezo wetu wa kufikiri na kuhoji nao umefikia rock bottom, naona tusubiri mabadiliko toka kwa kizazi kingine sio hiki chetu.
Wa kuikomboa bado awajazaliwa!"Huwezi kuikomboa nchi kwa kutegemea vijana wanao waza Pombe na Ngono"
~Che Guevara.