Watanzania maskini wametengwa na mfumo wa mabasi ya mwendo kasi (BRT)

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Asilimia 70% ya Watanzania ni maskini wanaoishi chini ya Tshs 4,400 kwa siku, halafu nauli ya haya mabasi yaani kwenda mjni na kurudi kitaa inagharimu Tsh 1,300 hivyo hiyo ni asilimia 30% ya kipato cha Mtanzania wa kawaida ambao ndio wengi hao 70%.
Wengi wameishia kuyaona yakipita tu lakini hawawezi kuthubutu kuyakaribia, kazi kuyapiga mapicha na kupost humu huku wakiwa wameketi kwenye daladala za kawaida.

Wabongo wasipokua makini hii ndio itakua taswira hata kwa SGR, kama watatumia gharama na nguvu nyingi kuirembesha kwa ajili ya kupiga mapicha kuliko unafuu wa huduma. Ni muhimu kuwakumbuka Watanzania 70% ambao hawawezi kukidhi haya mambo.
---------------------------------

Despite investments of $150 million for the first phase of BRT, the poor are still stuck in traffic on cheaper buses every day. By contrast, those who are wealthy enough to afford the higher fare have the option of cutting travelling time by two hours a day.
Roughly 70 per cent of Tanzanians live on less than Sh4,400 a day (less than $2). Yet a two-way commute along the main branch of the BRT would cost Sh1,300 – that’s a staggering 30 per cent of poor people’s daily income being spent on transport.
By comparison, the same commute by daladala would have cost Sh800
What’s more, the lack of jobs is a major problem in Dar es Salaam, as in many other metropolises in developing countries.
Since BRT buses can carry more passengers than minibuses, about 10 daladalas will be displaced by each BRT bus.
This will have devastating consequences for the 20,000 to 30,000 people employed in public transport.
Why BRT system excludes the poor
 
Kama mtu anaona hamudu hizo nauli arudi kijijini akalime tz bado in maeneo mengi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Nb:mbona ninyi li sgr lime double cost au ndio nyani haoni mkundu wake?

Futa hizo kauli, hakuna mtu hupenda kutoka kijijini kuja kuhangaika mjini hapo, kwanza kwa joto la Dar na harufu ukizingatia wengi wenu maskini mnaoishi mitaani hamuna viyoyozi au fan, ni mwendo wa kuvumilia joto na mijasho. Tatizo ni kwamba kijijini hakukaliki, umaskini umekolea kule, ardhi mnayo kubwa ila kama Waafrika wengine, bado mnatumia mbinu zilizopitwa na wakati za kulima kwa jembe.
Hivyo inawabidi mkusanyike Dar, ambapo mara ya mwisho nilisoma sehemu mumejazana watu milioni tano.
 
MK254 kuna pande mbili kwa kila jambo. Ni kweli kwamba kuna watu wameathirika kwa jinsi flan kutokana na hizo gharama lakini ni pia ni ukweli kuwa BRT imesaidia sana watu wengi. Wazia kwa mfano mwanzoni watu waliokuwa wanatoka Kimara kwenda Posta ilibidi waunge mabasi mawili au matatu kufika posta kwa kuwa daladala zilikuwa zinakata ruti sana. Kwa sasa ukipanda fasta umefika posta ama Kariakoo. Sikatai kuna changamoto nyingi bado ikiwemo Management ya huu mradi inayosababisha mrundikano wa abiria vituoni ilihali mabasi mda mwingine unakuta yamepaki tu(kwa mawazo yangu).Hayo ni mambo ya kufanyiwa kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata hizo gari zinausumbufu wake, ni heri kupanda gari za kawaida, hata wewe ukienda dukani kuna bidhaa tofauti kutegemeana na mfuko wako..

Ndio maana kuna watu wanapanda ndege, wapo wanao panda mabasi safari za mikoani..

Kila mbuzi atakula kwa urefu wa kambayake
 

Huyu aliyeandika hiyo analysis sijui alifikiria nini,
Hiyo $0.5 ya to and fro kwenye BRT ni coins za mkazi yeyote wa dar kwenye begi lake,
Kati ya changamoto zinazolalamikiwa na wakazi wa Dar gharama za nauli haipo kabisa,
Hapo ni umekurupuka mzee, brt ni usafiri wa kawaida sana na sio laxury kama mnavuodhani wakenya.
 
TSH 1400 is the petty money in Tanzania @
 
Wewe MK254 Major route Za mwendokasi hazina mbadala mfano,mkazi wa Kimara mwisho kama anataka kwenda CBD lazima apande mwendokasi tu hakuna mbadala,wenye option nyingine ni wale wanaokaa sehemu ambapo mradi haupo.
Pili wakazi wengi wa Dar wanakipato kikubwa kuliko maeneo mengine ya Tz kutokana na mzunguko mkubwa wa pesa jijini.

Mimi kabla sijahama Dar Nilikua nmeajiriwa nalipwa kwa mwezi Tsh 1M ni pesa ndogo tu lakini kuna wenye magenge yakuuza veges na zagazaga ndogo ndogo kwa siku hakosi tshs 50elfu faida ukimuona mchafu utamdharau lakin anapesa kuliko vijana wengi wale wa ofisini .Ni uongo uliotukuka mkaazi wa jijin akose 1300 ya nauli kwa siku wakati mtu uyo ananunua maji anakula mgahawani na bado ataweka vocha na bado nyumbani kwake ataacha pesa ya matumizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Sio kweli, nowdays Vijijini kuna fursa nyingi mno, watu wanakuwa matajiri kwa kufuga kuku tu, Imagine,
Kama ni kweli yupo mtu especially kijana yupo dar na hawezi kumudu hata nauli ya Mwendokasi walahi aende mikoani akajaribu maisha huko, hapa dar patakuwa pamemshinda.
 
Stedi huwa zimejazana watu kila saa kama mchwa..yani kusema hawa watu wote wapo vizuri kifedha..
Hapana wanapanda buree nawe sogea upande

{Hutajuta ukitembelea
& kusubscribe chanel yangu ya youtube jina Misifa Skills,Link hii hapa
 
Angalau ww nimekuelewa

{Hutajuta ukitembelea
& kusubscribe chanel yangu ya youtube jina Misifa Skills,Link hii hapa
 

Kufikiria kwako ni kawaida ya wadanganyika wenzako tu....Very lazy thinking
 
Inawezekana kwao ni luxury mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kweli kwamba Tsh.1300 ni coins za mkazi yeyote wa dar kwenye begi lake. Kuna watu wengi Dar wanatoa jasho kweli kweli kupata hio 1300 mfano waokota makopo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi mkuu mtaa wa mabanda hapo Nairobi hawajambo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…