Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Katika nchi ya watu wanaojifunza na kujiongeza, natumaini kadiri watu wanavyoweza kuchambua mambo kwa kina zaidi, ndivyo elimu itakavyoweza kupatikana, watu wajifunze kwa nuance.Mwisho wake ni nini?
1. Mazuri ya Magufuli ni yapi?
2. Mabaya ya Magufuli ni yapi?
3. Mambo gani tunaweza kufanya ili tusirudie mabaya aliyotuletea Magufuli?
4. Mambo gani tunaweza kufanya ili tujiongeze katika mazuri aliyotuletea Magufuli?
Bila kujua historia yetu, tumetoka wapi, kwa nini tumetoka hapo, na sasa tunakwenda mbele ya hapo au tunarudi nyuma, hatuwezi kupanga mipango vizuri.
Na maisha ya rais ni sehemu kubwa ya kuchambua historia yetu.
Kwa nini kumuongelea Magufuli liwe jambo la ajabu na linalopingwa?
Huyu ni mtu alikuwa rais wa watu zaidi ya milioni 60 kwa multiple presidential terms.
Magufuli anatakiwa kuandikiwa vitabu vya kuchambua maisha yake yote, tangu kifamilia, alivyosoma, alivyofanya kazi, alivyoingia katika siasa z abunge, alivyopata uwaziri, mpaka urais.
Kapanda vipi? Mfumo wetu umeruhusu vipi mtu kama huyu kupanda?