Watanzania milioni 7 wanakabiliwa na matatizo ya akili, 10% pekee wametibiwa

Watanzania milioni 7 wanakabiliwa na matatizo ya akili, 10% pekee wametibiwa

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Takwimu zilizotolewa na wizara ya afya ambapo watanzania milioni 7 wanakabiliwa na matatizo ya akili huku matumizi ya teknolojia kama mitandao ikiwa moja ya sababu iliyotajwa na wadau. Msongo wa mawazo pia ni changamoto nyingine inayokumba watanzania.

Wiki hii dunia inaadhimisha wiki ya afya ya akili ambapo kilele chake ni tarehe 10 mwezi huu ikiwa na lengo kuongeza uelewa na kukusanya nguvu kuboresha afya ya akili.
 
Takwimu zilizotolewa na wizara ya afya ambapo watanzania milioni 7 wanakabiliwa na matatizo ya akili huku matumizi ya teknolojia kama mitandao ikiwa moja ya sababu na wadau. Msongo wa mawazo pia ni changamoto nyingine inayokumba watanzania.

Wiki hii dunia inaadhimisha afya ya akili ambapo kilele chake ni tarehe 10 mwezi huu ikiwa na lengo kuongeza uelewa na kukusanya nguvu kuboresha afya ya akili.
Siyo kweli
 
Takwimu za kihuni na hii ni ishara ya kuumwa sonona.


  • Dalili ni pamoja na:
    • Hali ya msononeko au hasira wakati wote
    • Kupoteza hamu ya kufanya shughuli au mambo aliyokuwa akiyafurahia.
    • Hapati usingizi au analala sana
    • Mabadiliko makubwa ya hamu ya chakula, mara nyingi mgonjwa hupungua au kuongezeka uzito
    • Uchovu na kukosa nguvu
    • Mgonjwa hujihisi kutokuwa na thamani yoyote, hujichukia, na hujihisi mwenye hatia
    • Hupata ugumu kuzingatia mambo
    • Huwa mnyonge au mwenye papara
    • Hapendi kufanya lolote na huepuka kufanya shughuli za kawaida
    • Hujihisi kukata tamaa na bila msaada
    • Hupata mawazo ya kifo au kujiua mara kwa mara
    • Kutokujiamini ni swala la kawaida kwa mgonjwa wa sonona. Anaweza pia kuwa na hasira za ghafla na hukosa raha hata anapofanya mambo yanayopasa kumfurahisha mtu, hii ni pamoja na ngono.
    • Watoto wenye sonona huenda wasiwe na dalili sawa na watu wazima. Angalia mabadiliko kwenye kazi za shule, usingizi, na tabia. Kama unashuku mwanao ana ugonjwa huu, ni muhimu kuongea na mtoa huduma wa afya.
 
Uvutaji wa BANGI na ULEVI wa pombe wa kupindukia ni chanzo kikubwa sana cha kupata matatizo ya afya ya akili.
 
Back
Top Bottom