Watanzania milioni moja One MT project
Nimekaa nikifikiria kuhusu ujasiriamali nikajikuta naona mradi madhubuti ambao kama kweli, kwa nia moja na thabiti isiyo na chembe ya ufisadi inaweza kubadili kabisa mustakabali wan nchi yetu.
Watanzania milioni moja katika mradi huu kila mmoja anatakiwa kutoa US $ 1000, that sums up to US$ 1,000,000,000. Nikiwa kama mhandisi miradi niliyesimamia miradi mingi na yenye thamani mpaka kufikia US $ 400,000,00 ntajaribu kuiweka hoja yangu katika mtizamo huo.
Ieleweke kwamba tangu nchi yetu ipate uhuru hakuna mradi hata mmoja uliowahi kujengwa kwa gharama ya one billion US dollars na si hapa tu hata katika nchi zote za Africa miradi hiyo inahesabika. Hivyo basi that is a huge amount of money!!!!!!! Kumbe watanzania milioni moja
1.Tunaweza kujenga barabara ya lami ya kisasa kabisa kutoka Dar mpaka Mwanza.
2.Tunaweza kimiliki Liganga Mchuchuma kwa asilimia 100.
3.Tunaweza kujenga shule za kisasa kabisa say kwa US $500,000 each elfu mbili.
4.Tunaweza kujenga hospitali bora na za kisasa kabisa say kwa US $1, 000,000 each elfu moja.
5.Tunaweza kujenga bomba la maji kutoka Mwanza mpaka Dodoma na mikoa ya jirani
6.Tunaweza kujenga reli kutoka mtwara mpaka makambako.
7.Tunaweza kujenga PPF towers 200
8.Tunaweza kujenga bandari zote tatu kubwa sea ports (Dar, Tanga, Mtwara)
9.Tunaweza kumiliki mabasi yoote Tanzania.
10.Tunaweza kujenga mijengo ya Balali kwa bei halali kama mitano hivi.
11.Tunaweza kumiliki migodi yote iliyopo Tanzania kwa sasa
12.Tunaweza kujenga gas - power station Kubwa kuliko zote in East ,Central and Western Africa.
13.Tunaweza kuweka lami barabara zote za jiji la Dar.
14.Tunaweza kujenga viwanja vya michezo mithili ya ule wa mpya wa taifa kila moka
15.Tunaweza kuwa na capital kuliko fisadi yeyote hapa nchini.
16.Tunaweza kutoa ajira hizo milioni zilizo ahidiwa na JK.
17.Tunaweza kuunganisha mikoa yoote ya pembezoni mwa TZ kwa lami.
18.Tutakuwa tuna hela nyingi kuliko hata zile alizotoa Joji kichaka.
19.Tunaweza pia kununua Man U, Arsenal na Chelsea.
20.Tunaweza kufanya mengi tuuuuuuuu Kubwa zaidi hata yale Ambayo serikali imeshindwa kabisa kuyafanya toka tupate uhuru.
Truth: Watanzania milioni moja wanaoipenda nchi yao wanaweza kuiboresha nchi yao kwa mengi.
Challenge: Inawezekana kweli kukusanya watu milioni moja kuwauzia hii hoja ikakubalika na kutekelezeka?Who Hill manage this Project? Sounds not really uhhhh!!!!!
Ok lets work it out this way- Katika watanzania milioni moja, nusu yake yaani laki tano wawe ni govt fund. The remaining laki tano gawa kwa kumi = 50,000. Hivi haiwezekani kupata watanzania 50,000 wenye $10,000 kila mmoja tukatekeleza hii One MT project (One million Tanzanians project).
Nakaribisha mawazo na njia mbadala, we can work thru One MT project. Ninaamini tunaweza kufanya makubwa yasiyotarajika. Kama sikosei akina Mosha na ile NICO ni the same idea!!!!!!! Well but this is One MT project.
Nawakilisha.
Ku-spice majadiliano nitapingana na wewe. Kwanza tuanze na historical facts. Unaposema kuwa Tanzania haijawahi kuwa na mradi wa bilioni moja za kimarekani hiyo ni kweli kabisa.
Lakini ukichukulia billioni moja kwa thamani ya sasa na kama sio namba billioni moja, kuna uwezekano mkubwa ipo miradi iliyofika billioni moja.
Mradi wa TAZARA ulikuwa ni millioni 500 USD miaka ya 70. Na thamani yake kwa sasa inaweza kuzidi billioni moja USD.
Mradi wa ujenzi wa makao makuu Dodoma hauna hesabu za kueleweka lakini ukichukua time frame, kazi zilizofanywa za kujitolea na michango ya wananchi umezidi billioni moja USD.
Tukirudi kwenye mada. Analysis yako ni nzuri lakini kuna uwalakini mkubwa. Analysis nzima ime-base kwenye perception kwamba vitu hivyo vinawezekana. Lakini ukichukua kalamu na kufanya analysis ya watanzania wanaoweza kukupatia hizo 1000 USD na jinsi watakavyochangia hizo pesa, unaweza kuwa nyuma sana na matarajio yako. Na ukiangalia kwa undani sana, fikra zako hazina tofauti na yule aliyefikiria kuwa akiwaweka watu katika vijiji vya ujamaa watatoa mchango mkubwa wa kijiendeleza wenyewe na matokeo yake hakuna kilichofanyika.
Wapo zaidi ya watanzania 1,000,000 wanaotengeneza zaidi ya dollar 1,000 kwa mwezi au kwa mwaka. Lakini hizo pesa ni hizo hizo wanazotumia kuendesha familia zao na sio pesa za ziada au zilizopo katika akaunti ya akiba ambazo ungeweza kuzitumia kwenye miradi uliyotaja.
Umesema umeshawahi kusimamia miradi ya US $ 400,000,00 (I guess US $ 400,000,000). Ni uhakika kati ya miradi hiyo, ipo miradi iliyoendesha kwa mikopo kutoka benki. Kwa mtaji huu ningekuomba uachane na watanzania millioni moja na utueleze kama ungepewa mkopo wa dollar billioni moja ungeweza vipi ku-implement moja ya miradi uliyotaja na kuweza kuliletea taifa faida na kulipa mkopo?
Vilevile miradi mingi inakuwa underestimated na inapomalizika gharama zinakuwa kubwa kuliko kiwango cha mwanzo. Kwa mfano, Euro Tunnel kuunganisha UK na Ufaransa ulikuwa ni mradi wenye makadirio ya Paundi chini ya 5 Billioni. Na ulipomalizika ulitumia Paundi Billioni 10. Na kwa sasa hivi faida inayopatikana katika mradi huu haiwezi kulipa interest ya deni la mradi huu.
Kwa mfano wa Euro Tunnel. Ikitokea kwamba umechukua pesa za watanzania millioni 1, lakini katika ya maendeleo ya mradi au pale mradi unapomalizika inaoneka kuwa pesa zilizotumika ni mara mbili au tatu kuliko makadirio yako ya mwanzo ni njia gani utatumia kuondoa matatizo yatayojitokeza kama vile madeni?