Bin Maryam,
Now this is much better as far as constructive criticism, goes.
Nyambala katoa Fikra, Umetoa utaalamu pinganifu, let the game begin.
Your analysis puts us into thinking mode on how to realize this Dream of Nyambala. Huku ndiko kulikuwa kunahitiajika ili kujenga mradi madhubuti na si kuanza kuogopa na kutafuta visingizio kuwa mradi hautafanikiwa.
Rev:
Naona katika mijadala kama hii nywele zako uwa zina-sisimka. Pingamizi langu kubwa sio hoja ya kukataa
Mawazo ya Mwanzilishi ndugu Nyambala. Pingamizi nililonalo ni risk-factors ambazo zinaambatana na miradi iliyopo katika
mazingira yetu na mitigation zake.
Ukweli wa mambo baada ya uhuru serikali nyingi za kiAfrika zilijiingiza katika juhudi za industrilisation.
Vikwazo vikubwa vilikuwa business model walizofuata, mismanagement, matapeli wa kimataifa ambao walitumia
naivette ya waafrika kuiba pesa kwa kutoa miradi iliyowanufaisha wao na sio waafrika na mambo mengine.
Kushindwa kwa kujaribu sio kitu kibaya iwapo utajenga Knowledge base ambayo itasaidia kuondoa matatizo ya miradi iliyopita
na kujenga Excellency ya uanzishaji na uendezaji wa miradi inayokuja.
Katika posti zilizopita. Kuna mtu alisema Nyerere alianzisha University lakini Mwinyi na Mkapa walishindwa.
Fundi Mchundo (Fundi Mwenzangu) akajibu kwa kusema kuwa kuanzisha sio kazi, kazi ipo kwenye kuendeleza. Na kwa wale
waliopitia IT, wanajua kabisa kuwa implementation ya IT system ni 20% ya bajeti na maintanance ni 80% ya bajeti. Na kwa mtaji
huu kila mradi una implementation cost na running cost.
Mpaka sasa watanzania wamesha-implement miradi mingi tu. Hivyo kwa sehemu kubwa weakness yetu haipo katika kubuni
miradi au kuanzisha. Weakness kubwa ipo kwenye kuendesha miradi hiyo (running). Na siku zote usiendeshe kitu kwa kutumia weakness
zako. Utapata hasara tu.
Hivyo wazo la mtu kutumia mchango wa watanzania 1,000,0000 kuanzisha mradi sio kitu kibaya lakini hiyo ni 20-40% ya mradi mzima.
60-80% ni sehemu ya ku-run au kuendesha mradi mzima ili ulete manufaa.
Hivyo changamoto kwa watoaji wa mada inabaki palepale. Watueleze wataleta utamaduni upi wa kuongoza miradi hiyo hili itoe faida
kwa waliochangia na kwa jamii.