Watanzania mkifika nje ya nchi jiandikisheni Ubalozini. Ona lawama kibao kwa Serikali wakati Ubalozi haujui kuwa wengi mko Ukraine

Lazima kuwe na coordination ya mifume ya ufanyaji kazi

Ni jukumu la serikali kuwa trace raia wake wanapokuwa nje ya nchi

Mambo ya kwenda kujiandikisha ni mambo ya kizamani...
Mkuu mifumo mingi ya Serikali haisomani Waziri mkuu aliongea kwa uchungu sana hilo
Hebu fikiria NIDA na Kitengo cha Passport ni chini ya wizara moja ya mambo ya ndani lakini mifumo yao haisomani wakati kampuni za Simu ambazo zina mifumo yao hiyo yao inasomana na NIDA unaweka kidole tu taarifa za NIDA hizo kitengo cha Passport mfumo wao haisomani na NIDA wakati wizara ni moja system zimekuwa developed na wizara hiyo hiyo halafu hawasomani!!
 
Hio shida kubwa sana

Wizara kuongozwa na watu wasio wabunifu wao wanawaza piga porojo kuzima kelele za wanachi wenye madukuduku.

Katibu mkuu wa wizara mzee aliepitwa kushoto na technolojia.

Yaani kuomba passport haikupaswa hata kupeleka taarifs yoyote toka kwangu labda picha yako sasa maana taarifa zetu NIDA wanazo

Ni swala la kuchota hapa kuweka kule

Hii nchi tabu sana
 
Hio shida kubwa sana

Wizara kuongozwa na watu wasio wabunifu wao wanawaza piga porojo kuzima kelele za wanachi wenye madukuduku...
Viongozi wapya wizara ya mambo ya ndani wameanza vizuri kuna mambo wameanza vizuri sana kutatua Kero

Hilo walifanyie kazi kuhakikisha NIDA na kitengo cha Passport system zao zinasomana ni abuse kuona kampuni za Simu zaweza somana na NIDA halafu kitengo cha Passport ndani ya wizara hiyo hiyo hawawezi kusomana wao kwa wao ofisi moja!!
 
Siyo hazisomani zinasoma vizuri sn sema shinda ni urasimu kila upande unataka kupiga pesa kivyake, hivyo ni vitengo vya watu mkuu
 
Siyo hazisomani zinasoma vizuri sn sema shinda ni urasimu kila upande unataka kupiga pesa kivyake, hivyo ni vitengo vya watu mkuu
Anyway wanajilimbikizia mipesa ya dhuluma utafikiri wataishi milele na hiyo mipesa at the expense of wananchi

Mungu yupo.Mungu sio Mzee Athumani
 
W
Watu wengi hawana exposure ndio maana wanajisemea tu. Yaani mtanzania afike Ukraine then aanze kuprocess visa na kuanza safari ya kwenda Sweden?

Hizi balozi ni nadra kujibu hata email.

Watu wanaona Ubalozi wa Marekani unavyotoa alert kwa wamarekani wawapo nchini wanafikiri kila nchi iko level moja! USA wana data za wananchi wao wakiwa ndani au nje ya USA.
 
Hii huenda ikawa ni miradi ya watu ya kupiga pesa. Huenda mfumo wa Passport ungeboreshwa kidogo tu ukabeba sehemu ya kutoa vitambulisho va NIDA tena kwa gharama ndogo. Mimi sijui ila maguru wa fani hii waweza sema.
 
Watanzania mkifika nje ya nchi jiandikisheni ubalozini ona sasa lawama kibao kwa serikali wakati ubalozi hauwajui wengi wenu kuwa mko Ukraine serikali iwasaidieje wakati mliingia kimya kimya kama vibaka...
Waulize walioko huko watakuambia jinsi mabalozi wanavyowakimbia, huwa hawana msaada wowote.
 
Watanzania mkifika nje ya nchi jiandikisheni ubalozini ona sasa lawama kibao kwa serikali wakati ubalozi hauwajui wengi wenu kuwa mko Ukraine serikali iwasaidieje wakati mliingia kimya kimya kama vibaka...
Tatizo liko kwenye hizo ofisi za ubalozi! Mtanzania ukienda huko ubalozini utajuta kwa nini ulienda huko. Ukifika getini mlinzi akakuuliza shida yako na yeye kuipeleka ndani, jibu atakalokuja nalo utaapa kutokurudi tena hapo ubalozini. Kitu wanachowaza haraka ukijitambulisha ni kuwa unataka kuomba msaada kitu ambacho hawataki kabisa kujisikia.

Na kwa bahati mbaya ukipata matatizo ndiyo kabisa hawana mpango wa kukusikiliza. Sasa kuna sababu gani kwenda kutoa taarifa hapo. Mara mia kwenda kuripoti ubalozi wa Uingereza katika nchi ambazo Tanzania haina ubalozi utasikilizwa.

Ubalozi pekee ambao nikiri niliwahi kupata ukarimu wa hali ya juu ni Zimbabwe wakati General Mboma akiwa mwambata wa jeshi pale ubalozini. Kiukweli mimi ndiye nilitafutwa na ubalozi kwa kuwa binafsi sikuwa na mpango wa kwenda ubalozini.
 
Watanzania mkifika nje ya nchi jiandikisheni ubalozini ona sasa lawama kibao kwa serikali wakati ubalozi hauwajui wengi wenu kuwa mko Ukraine serikali iwasaidieje wakati mliingia kimya kimya kama vibaka...
Nchi ambazo tu kuna balozi za Tz, watu wanakaa kinyemera sembuse hiyo ukraine ambako ubalozi wa Tz, uko swiden?!!na hata ujiandikishe kwenye mazingira yetu, usitegemee msaada mkubwa sana!kama hapa S.Afrika tu, mtu amepata matatizo anaenda ubalozini anaambiwa jinsi ulivyokuja ndiyo hivyo hivyo urudi TZ!!hatuna msaada!

Kuna nchi zinapenda raia wake bnana, hadi mtu unaona raha kuwa na utaifa wake! Na huko ukraine tatizo jingine hata ukituma ndege POLAND, unaweza ukaondoka na watz 7 tu, kwani kila mtu yuko kwenye chimbo lake, huko ukraine, kufika poland inategemea na jinsi putin alivyo litaiti eneo hilo!!!
 
Watanzania mkifika nje ya nchi jiandikisheni ubalozini ona sasa lawama kibao kwa serikali wakati ubalozi hauwajui wengi wenu kuwa mko Ukraine serikali iwasaidieje wakati mliingia kimya kimya kama vibaka.
Kuwalaumu watanzania ni kuwaonea, kwanini hawakuambiwa huku nyumbani kabla hawajaondoka, why revert the wheel to the victim now?
 
kama hapa S.Afrika tu, mtu amepata matatizo anaenda ubalozini anaambiwa jinsi ulivyokuja ndiyo hivyo hivyo urudi TZ!!hatuna msaada!!
Ngoja twende Taratibu unataka ubalozi ukupe inauli au? Ndugu zako Tanzania wote walifariki dunia hawawezi kuchangiana wakupe tickets au? Msaada gani unataka ubalozini ? Fafanua wazi
 
Watu hawajuani hata na mabalozi wa nyumba kumi humu nyumbani ndio itakuwa huko kwa wazungu?
Una hoja anamjua balozi Siku kadakwa anahitaji dhamana mahakamani! Ya ndiguye au yake!! Siku zingine anajifungia ndani ya geti na kutembea gari vioo vimefungwa tinted kila kona!! Mheshimiwa huyo hahitaji kumjua mtu mdogo kama balozi wa nyumba Kumi hata jina anaitwa nani!

Akienda nje anaendekeza hiyo tabia
 

Hili ni tatizo la kinchi kabisa kuanzia humu ndani. Usishangae hata hao mabalozi wetu huko nje, hawajui viongozi wao wa mitaa wanayokaa humu nchini!
 
Kwahiyo unamaanisha ofisi ya uhamiaji Tz hazina mawasiliano na ofisi za ubalozi?
 
Watanzania mkifika nje ya nchi jiandikisheni ubalozini ona sasa lawama kibao kwa serikali wakati ubalozi hauwajui wengi wenu kuwa mko Ukraine serikali iwasaidieje wakati mliingia kimya kimya kama vibaka...

Ubalozi wenywewe uko Sweden alafu unatakiwa kuhudumia mataifa kibao. Ufanisi wa ubalozi nao ni wa mashaka ukijumlisha na urasimu.

Suala siyo tu kujiandikisha pekee. Je jamuhuri inawathamini na kuipa uzito raia wake kiasi gani?
 
Anyway wanajilimbikizia mipesa ya dhuluma utafikiri wataishi milele na hiyo mipesa at the expense of wananchi

Mungu yupo.Mungu sio Mzee Athumani
Mwisho wa siku haya majangili ndiyo yanategemewa kwa misaada kanisani na yana tupu tena kwa msaada wa viongozi wa dini.
 
Mtoa mada katoa hoja nzuri ( ingawa mwandiko kama wa bata). Wachangiaji wengine sasa, wanatoa hoja mfu na miandiko ovyo.
Tusameheane miandiko hatufanani angalia hoja hata kama inaeleweka asilimia mbili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…