Watanzania mliopo hapa Kampala Uganda mnawezaje kula Mdudu (Kitimoto) cha hapa kisicho la ladha kama ya kwetu Tanzania?

Wana mapishi ya ajabu chapati, wanakatia maharage kisha unakunywa na uji wa ulezi.
Juzi kuna Mganda Mmoja ndiyo Kanishangaza yaani nimemwambia anipe Chapati na Mayai Yeye ( nadhani kwa Mapishi yao huku ) akaichanganya ile Chapati na Yai baada ya Kulikaanga kisha akanipa na wala sikuifurahia sema Njaa tu niliyokuwa nayo ilinilazimu niile huku Uso wangu ukiwa na Usununu / Hasira. Ni kweli kwenye Kupika wapo nyuma mno na Tanzania tumewaacha mbali mno.
 
Ukiona alosto ya kitimoto inazidi panda kagari hapo vuka hapo mutukula mara moja ifinye upande wa pili rudi achana na ya mmachame kale ya nshomile
 
Ukiona alosto ya kitimoto inazidi panda kagari hapo vuka hapo mutukula mara moja ifinye upande wa pili rudi achana na ya mmachame kale ya nshomile
Labda asogee mpaka bk huko mipakani hawachekani na waganda kiufupi ndo wale wale
 
Ila bora kidogo huko,,,Kenya ndo funika bovu, kuna siku nimeamka na hangover nikaomba supu kwanza nashangaa naletewa kwenye kikombe kama chai halafu kikombe cha bati na ndani wamekuwekea hio supu sijui wamechanganya na mafuta gani,haina nyama hata 1 na ladha ya ajabu, mhudumu akaweka mezani halafu akasepa nikabaki natoa macho tu kuonja sikuiweza nikaacha ikabidi niende tu kwenye nyama ya kuchoma,,,,,kwenye wali ndo kabisa kenya usiagizie labda kama umeenda migahawa ya wasomali au watu wa pwani
 
MKUUU NIMRTOKA MWEZI JANA HAPO NTINDA NDUGU KUNA MASSAWE MMOJA KAJIPANGA NA KINA MUSHI WANAPIGA HELA SEMA TU WALE MADADA KUHUDUMIA WATEJA KIDOGO SHIDA
Ogambaki Ssebo
 
Kuna binti tulisoma nae baba yake alikuwa ni afande mkubwa huku lakini vitu tulivyokuwa tunafanya nae basi hakika yule mzee angetupa kesi ya uhaini.

Ila maisha ya Kampala ya 90's na early 2000s yametufundisha mengi sana katika dunia ya leo.
Sure. Umenikumbusha mbali. Ule mchanganyiko wa wakikuyu, jaluo, karamajong, Baganda, wabongo, wanyarwanda, NK ulitufunza mengi
Michemsho ya karanga daily nayo inachosha ujue
Binyebwa. Dah long time
 
Kuna binti tulisoma nae baba yake alikuwa ni afande mkubwa huku lakini vitu tulivyokuwa tunafanya nae basi hakika yule mzee angetupa kesi ya uhaini.

Ila maisha ya Kampala ya 90's na early 2000s yametufundisha mengi sana katika dunia ya leo.
hicho kipindi cha Muduuma na mukono huko migombani πŸ˜πŸ˜„
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…