Mkuu ukisema statistics unamaanisha unapotoa matokeo unasema umepima wangapi ? umepata wangapi na ugonjwa na wangapi hawana ugonjwa , hapa tatizo sio sisi tupo ahead tatizo kipimo kipo daslama tu, hata makao makuu ya nchi dodoma hakuna hicho kipimo, nchi nzima corona inapimwa muhimbili tu sasa hilo ni tatizo kubwa kwa nchi kama tanzania watu wengine labda wanajifia tu huko bila hata kujua kama ni korona au la na wanazikwa kama kawaida sasa hilo ni tatizo mkuu
Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu sio kweli unalosema, tatizo ni kwamba lazima uwe unajua lengo la kufanya hivyo vipimo.
1) Kama unataka kujua ni watu wangapi nchini mwako wameambukizwa ugonjwa, haina maana yoyote ya kutafuta "denominator", ndio sababu unasikia idadi zinazotangazwa na WHO za maambukizi duniani kote, kamwe hawataji idadi ya watu waliopimwa, wanataja wenye maambukizi na vifo.
2)Kulinganisha watu waliopatikana na ugonjwa " numerator " kwa watu waliopimwa " denominator", ni muhimu tu kama unataka kujua ni kwakiasi gani huo ugonjwa umepenya katika nchi husika, kwa ajili ya matumizi ya kiofisi na kiserikali kupanga bajeti zao na mipango yao. Hii haijalishi umepima watu wengi kiasi gani, unaweza kuchukua "sample size" yoyote na ikakuonyesha ni kiasi gani ugonjwa umepenya nchini mwako.
3) Sasa hivi katika janga kubwa kama hili, muhimu ni kuzuia maambukizi yasisambae zaidi, na kupunguza vifo na athari za kiuchumi na kijamii zinazosababishwa na Corona, hakuna faida yoyote ya kujua umepima wangapi, muhimu ni kujua walioambukizwa ni wangapi na nini kifanyike ili wengine wasiambukizwe zaidi. Nchi zote duniani zinaweka mkazo katika kutumia dalili badala ya kupima.
4) Hakuna nchi hata moja yenye vituo vya kupima Corona kila sehemu, kama nilivyosema na kumsikiliza hiyo Daktari mtanzania aliyeko UK, nchi za Ulaya hazipimi wagonjwa wa Corona, kwahiyo hawana sababu yoyote ya kujenga maabara kila sehemu. Unahitaji maabara chache sana, ila unahitaji mipango na mikakati ya kuzuia na kutibu wagonjwa.
5)Hao wakenya wasikudanganye, wanazo maabara mbili tu, tens zote zipo Nairobi, tatizo lao kubwa hawajui nini wanapaswa kufanya, ndio sababu hata Nzige wamewashindwa kuwadhibiti, usitegemee lolote wataweza kudhibiti Corona, hao ni mdomo tu, hawana lolote.
Sent using
Jamii Forums mobile app