Watanzania mnaopenda kuja Norway kutafuta maisha chukua ushauri huu, kazi nyingi ni za bandarini

Watanzania mnaopenda kuja Norway kutafuta maisha chukua ushauri huu, kazi nyingi ni za bandarini

Huyu jamaa analipwa minstelønn au minimum wage kama wanavyoita wenyewe. Lakini akija Mzungu kutoka Sweden, Poland au Lithuania, Temporary Agency watawalipa hao Wazungu zaidi kwa saa kwa kazi ileile sababu ni Wazungu, achilia mbali Wenyeji ambao huwa wanalipwa zaidi kwa saa mara zote ukilinganisha na Wahamiaji kutoka Africa.
Brother upo deep sana..!
 
Bidhaa wanazozalisha huku kwa Tz hazina soko na pia bidhaa za huku Hadi zifike TZ zitakuwa Bei juu Sana
Wewe nenda Asia, huko ndio kwenye dampo la Tz
Sikutegemea kama akili yako ingewaza hivi na exposure yote hiyoooooo. Kuna groceries fresh nyingi snaa hutumwa na ndege kuja huko Scandinavian countries kila uchwao...... panua akili na mawazo yako ufike mbaliiii.
 
Sishauri kwenda norway kwa watu wasio na pesa ya kutosha. Maisha ni ghali sana. Speaking from experience. Toka una mpunga uende hujo.
 
Waswahili wenzangu huwa wanapenda kusema kizuri kula na nduguyo.

Najua wengi tu wanapenda kuishi Europe, pengine sio kwa sababu ya ugumu Sana uliopo bongo Bali ni sababu ya maisha ya huku yalivyo.

Nitaongelea zaidi Norway kwa kuwa ndio nipo.

Kwanza kabisa ugumu upo popote pale hivyo usije unafikiri ukifika huku kazi yako ni kula naa kulala tu, hapana. Huku ukija jua kuwa utaafanya kazi haswa ili upate kipato. Hakuna Cha bure bure.

Ni lazima uwe tayari kufanya kazi mbalimbali za day worker(deiwaka) na usichague.

Kazi za huku za deiwaka zinalipa Sana kwa kuwa wao hawazipendi hivyo kufanya mahitaji ya kazi hizo kuwa makubwa.
Uaminifu.

Hawa wenzetu wanapenda Sana uaminifu, usije hata siku moja ukathubutu kuiba au kuchelewa kumaliza kazi bila sababu za msingi.

Huku Kuna bandari nyingi Sana hivyo kazi za bandari ni nyingi Sana, ieleweke usitake kujifanya una degree. Hakuna anayeitambua huku, wewe huku njoo Kama vile hujawahi kusoma Wala kuwa na degree, Cha msingi onesha ufanisi kwenye kile unafanya.

Kuna baadhi humu Ni wajuaji Sana anakuambia naijua Sana Norway hakuna kabisa pesa.

Ndugu yangu dunia nzima hakuna pesa Ila inategemea wewe unaitafuta vipi.

Narudia tena huku pesa ipo Ila sharti uitumikie haswa.

Kutokana na uaminifu wangu mkubwa nimebahatika kupata kazi/vibarua sehemu tofauti na vinanilipa vizuri tu.

Sasa hivi Kuna kazi/kibarua nimepata kwenye moja ya bandari huku na nitakuwa nakunja pesa nzuri tu.

Mimi sio mzuri Sana wa negativity, always nipo positive. Hivyo namaanisha kuna mabaya nayaona si unajua ngozi nyeusi tunadharaulika Sana Ila sio vitu vya kujali hata kidogo. We piga kazi

Kwa wale wote mnaopenda kwenda ulaya kutafuta maisha hasa Norway chukueni ushauri huu.

Niliona maswali watu wanauliza nilifikaje, nadhani Hilo nililikatisha sababu ya kutukanwa na kuandamwa bila sababu.

Lakini Kama unatamani kuja huku fanya hustle zako vizuri njoo, Wala msikatishe watu tamaa. mwenye kutaka kuja aje Ila usikubali kuingizwa mjini au kutapeliwa na Mtu yoyote kwa kigezo cha kukusaidia pambana mwenyewe mwanzo mwisho, inawezekana kabisa ukafanikiwa bila msaada wa Mtu.

inshaallah nitafika mkuu hapo norway
 
Back
Top Bottom