Nina Akili Ndogo Sana
JF-Expert Member
- Jun 2, 2026
- 865
- 1,125
NB: Nina Akili Ndogo Sana
Kabla ya vurugu na mauaji ya Oktoba 2025, TCRA waliwahi kuchezea mifumo ya utendaji kazi pale ofisi zao kuu za Dar Es Salaam kisha nikawaandikia ujumbe huu wa barua pepe pasipo mimi kujua kama Kuna balaa linakuja mwezi wa Oktober.
====
Habari za wakati huu,
Ndugu zangu.
Bila shaka mpo wazima kabisa wa afya na poleni sana kwa shughuli za ujenzi wa taifa.
Ndugu zangu wote mtakaopata bahati ya kuusoma ujumbe huu wa barua pepe, ninaomba, kwa heshima na taadhima, kuwakumbusha jambo moja tu ambalo ninahisi watu wengi aidha wamelisahau au hawana elimu ya kutosha juu ya suala hilo.
Kwa yeyote nitakayemkwaza, kwa namna moja ama nyingine, nitaomba anisamehe sana.
Ndugu zangu;
(1) Usalama na ustawi wa Taifa la Tanzania sio jukumu la CCM pekee.
(2) Usalama na ustawi wa Taifa la Tanzania sio jukumu la CHADEMA pekee.
(3) Usalama na ustawi wa Taifa la Tanzania sio jukumu la ACT peke.
(4) Usalama na ustawi wa Tanzania sio jukumu la CUF peke.
...bali, usalama wa ustawi wa Taifa letu pendwa la Tanzania ni jukumu la kila mtanzania mwenye mapenzi mema na Taifa hili pasipo kujali itikadi zake za kisiasa (Political Affiliations), dini, kabila, rangi au maumbile yake kwa ujumla.
Ndugu yangu mzalendo, pindi uonapo mifumo au taasisi za serikali (mfano CMA, TCRA au Polisi) inalegalega katika kutimiza wajibu wake ipasvyo, usikae kimya, bali amka upaze sauti mpaka viongozi waandamizi wa nchi au taasisi husika wapate kujua.
Ndugu yangu, kamwe tusiruhusu watumishi waliokosa uadilifu kama ******* wa TCRA Dar Es Salaam wakatuharibia taasisi zetu zilizokuwa imara miaka nenda rudi.
Kupaza sauti yako sio tu kwa manufaa yako pekee, hapana, bali kwa manufaa ya watoto pamoja na wajukuu zetu miaka 50 ijayo au zaidi.
(A) Mifumo/taasisi zililegalega nchi Rwanda mwaka 1994, na sote tunajua nini kilitokea.
(B) Mifumo ililegalega nchini Kenya mwaka 2007, na sote tulishuhudia ile kadhia.
(C) Mifumo ililegalega nchini Liberia kipindi cha Charles Taylor na Samuel Doe, we all witnessed that chaos.
(D) Mifumo ililegalega nchini Somalia wakati wa Mapinduzi yaliyoongozwa na Major General Syad Baree, tuliona ya kutisha.
(E) Mifumo ililegalega nchini Nigeria wakati wa utawala wa Ibrahim Babangida pamoja na General San Abacha, mambo yalikuwa mazito.
Mifano yote hapo juu ilitokea kwa sababu walalahoi kama mimi Edward walikaa kimya pasipo kupiga kelele ndani ya nchi zao.
Ndugu zangu, kamwe tusiruhusu mifumo kama ya Polisi, CMA, TCRA au taasisi yoyote ile ya umma ikalegalega kwa maana, hatupo tayari kulipa gharama kubwa kwa uzembe wa watumishi wachache wa serikali wanaotumia vibaya madaraka yao.
We shouldn't allow the law of the jungle (survival of the fittest) to take hold, prevail and undermine our very systems which were once strong and we, all, used to relay upon, simply because we were way too complacent to hold to account some few officials who were trying to sabotage their effectiveness.
KUMBUKA: Jahazi Tanzania likizama, tutazama wote. Jahazi Tanzania likineemeka, tutaneemeka sote.
The choice is all ours to make.
Ni mimi MPIGA DEBE Mlalahoi,
Dar Es Salaam,
Tanzania.