Watanzania msifanywe Chuma ulete na hawa Wasanii au watu wenu Maarufu

Watanzania msifanywe Chuma ulete na hawa Wasanii au watu wenu Maarufu

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
14,762
Reaction score
32,386
Wakiwa na pesa huwa wala hawawakumbuki. Wanatamba na kuonesha jinsi ambavyo wanafaidi maisha na nyie sababu wavivu mnataabika.

Daily wanapost wakila kuku, wakiwa dubai, china na ulimwenguni waki enjoy life. Wanakula maisha wanapewa na chama chakavu maishani. Wakianza kuumwa pesa zao hawataki kutumia.

Wanaanza kuwaambia muwachangie. Yaani matibabu wanataka watumie pesa zenu nyie maskini ambao mkiumwa hata Muhimbili tu kutibiwa kitendawili. Ila wao wanataka wakatibiwe INDIA.

Nyie mkatibiwe Mtogolwe Dispensary wao wakatibiwe India na South Afrika. Wakirudi wamepona wanaanza tena kuwatambia na pesa zao na zenu zilizobaki. Acheni ujinga na kufanywa chuma ulete.
 
Back
Top Bottom