Watanzania msipotoshwe na hoja za kiukaguzi (Audit queries) maana sio hitimisho kuwa ni ufisadi, zikipatiwa majibu ukweli hujulikana

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Huu ni utaratibu wa kawaida katika kufanya ukaguzi wa matumizi, au taratibu za ujenzi. Kwamba mkaguzi ataibua hoja ya kuwa na wasiwasi juu ya anachokagua pale panapotokea kuwa hakuna vielelezo vya kile anachohoji ili kuthibitisha. Hivyo baada ya kuibua hoja hizo majibu ya uhakika huwa yanahitajika.

Mfano mkaguzi anakagua juu ya manunuzi ya sare za jeshi la polisi, lazima aulizie risiti za manunuzi, usafiri na ikiwezekana aone hizo sare. Asipoziona hapo ndipo huibua hoja ambazo huhitaji majibu.

Kwa hiyo kama CAG ameibua Audit queries sio conclusion kuwa tayari kuna ufisadi. Maana lazima PAC au LAAC watafute majibu ya hizi hoja ili tujue ukweli wake.

Hivyo wanasiasa wapenda sifa kama Zitto wasitumie nafasi hii kupotosha umma kuwa tayari kuna ufisadi.

Mmesahau ishu ya tril 1.5 ambayo ilikuja kupata majibu? Mbona Assad hadi hii leo na hasira zake za kufukuzwa uCAG hajaikumbushia kama kweli zilipigwa.

Tusubiri majibu ya PAC ka LAAC.
 
Kigwangala bhana! Yani ule utani pale Serena ukaandika kweli humu. Najua nimekuudhi.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Muoneeni huruma jamani
 
Una hoja tena hoja yako ni sahihi kwa sababu umeeleza hatua tu zinazofuatwa baada ya Audit Query kuibuliwa na CAG. Lakini bado hoja hiyo haifuti uwezekano wa kuwepo ufisadi. Kwa taarifa yako mpaka sasa kuna Mawaziri wameshachukua hatua dhidi ya Watumishi walio chini ya Wizara zao ambao Idara/Vitengo vyao vimekutwa na hoja za Kikaguzi.

Hoja yako nyingine kuhusu 1.5t kuzimwa na PAC na shambulizi lako dhidi ya CAG aliyefukuzwa kazi Prof. Assad, umejaribu kutetea uozo na huku ukijua ndoa haramu kati ya Bunge na Serikali. Ni nchi gani uliona Bunge linakuwa na kazi ya kusafisha kashfa za Seriakli?

Danadana zilizopigwa kuhusu fedha hizo tunazikumbuka sana labda wewe ndo umejisanaulisha, mara ziko Zanzibar, mara ni makosa ya kiuandishi, mara blabla.
 
Huyo mrembo wa TTB akija kubainika hana kosa? Kusimamishwa kazi sio kuwa amehusika.

Sijatetea uozo, wala kushabulia mtu. Ukweli ni kuwa Assad aseme ukweli juu ya tril 1.5, tujue kama PAC walitudanganya.

Lakini ukweli ni kuwa majibunya CAG hujibiwa na PAC au LAAC. Kama huwa wanafanya uhuni basi sasa hapo ni mengineyo.
 
Kwahiyo wale wa hati chafu nao tuseme wameonewa flani hivi?

naposema 1.5T zilikuja kupata majibu, UNAWEZA UKATUWEKEA HAPA HAYO MAJIBU? Maana binafsi sikuwahi kuyasikia majibu halisi, ila akina Polepole kujaribu kutueleza mara Zanzibar, mara sijui nini!

HAYO MAJIBU KWANINI HUWA HAWAMPI CAG wakati wanaulizwa? Kwanini ripoti ikishatoka na mnahangaika kumjibu CAG?

Kwani hao wanaoulizwa hayo makitu, huwa hawapewi nafasi ya kueleza au kutoa uthibitisho wa wanayoyasema? Hivi waulizwaji si wanajua kuwa kuna time frame ya wao kutoa majibu na ukivuka wakati huo maelezo yako yanakuwa hayana maana?

NI SAWA NA HUKUMU ILYOTOLEWA MAHAKAMA I INA MUDA WA KUKATIWA RUFAA, MUDA UKIPITA YALIYOAMULIWA YANABAKI KUWA NI MAAMUZI SAHIHI.

HUWEZI SUBIRIWA FOREVER
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…